picha
ikionyesha wafanyakazi wa NSSF pamoja na mganga mkuu wa hospitali ya
wilaya ya Tengeru katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada
wa vyandalua
wafanyakazi wa NSSF wakiwa wanabadilishana mawazo nje ya hospitali hiyo
mmoja ya wagonjwa akiwa amekaa kitanda kimoja na watoto wawili wakiwa kila mmoja ana mama yake
Na Woinde Shizza,Arusha
Hospitali
ya wilaya ya Tengeru (Patandi) inakabiliwa na ukosefu wa vitanda hali
ambayo inapelekea wagonjwa kulala zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi hili wagonjwa hao mara baada ya kupokea
msaada wa vyandalua kutoka kwa wafanyakazi wa mfuko wa hifadhi ya jamii
(NSSF) tawi la Arusha walisema kuwa wao kama wagonjwa wa hospitali hiyo
wamekuwa wanapata tabu sana haswa wakati wakiandikiwa kulazwa kwani wana
banana sana na wakati mwingine wanakosa kabisa vitanda.
Mmoja
wa wagonjwa hao ambaye alijitambulisha kwa jina la Anna Akyoo alisema
kuwa wamekuwa wakilala wagonjwa wawili hadi watatu hali
ambayo inawafanya wajisikie vibaya kwani wana banana sana katika
vitanda hivyo vichache.
Unajua
mfano mimi nimekuja hapa unaniona nipo na mtoto wangu lakini tunalala
wawili kwaiyo ukichanganya na watoto wetu maana unaona hii ni wodi ya
mama na mtoto tunakuwa wanne kweli tunaomba sana serekali ituangalie
sana hospitali hii kwani tunateseka nasio kuteseka tu sasa tunavyobanana
hivi muda mungine tunaweza ata kutoka na magonjwa mengine umu,unakutwa
umemleta labda mtoto anaumwa ugonjwa huu tukija apa huku kubanana badala
ya kupona anatoka na gonjwa lingine kweli watuangalie sana”alisema Lea
Mmari'
Kwa
upande wake mganga mkuu wa hospitali hiyo ya wilaya ya Tengeru Ukio
Kusirigwa alisema kuwa ni kweli tatizo la vitanda lipo lakini sio kubwa
kikubwa kinachowakabili hospitali hiyo ni kukosekana kwa wodi
za kuwalaza wagonjwa hali ambayo inawafanya wawabananishe katika
vitanda hivyo.
“unajua
siwezi sema kuwa tatizo la ukosefu wa vitanda hamna hapana lakini shida
kubwa ata tukipata vitanda sasa ivi tutaviweka wapi na wodi zimeja
,hospitali hii ya wilaya imekuwa inapokea wagonjwa wengi kutoka tengeru
hapa ,mererani na ata kia na kikatiti maana hii ndio hospitali kubwa ya
wilaya iliopo karibu hivyo kwa wingi huo na ukiangalia wodi ni chache
tunakosa jinsi hivyo inatubidi wagonjwa walale wawili wawili ili waweze
kupata huduma”alisema Kusirigwa.
Aidha
aliwaomba wadau pamoja na serekali kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kama
vile wafanyakazi wa NSSF tawi la Arusha walivyojitokeza kuja kutoa
misaada angalau ya vitanda,majengo na kikubwa zaidi aliwaomba sana
waisaidie hospitali hiyo kujenga wodi kwa ajili ya wagonjwa wakiwemo
wakina mama na mtoto.
Naye
meneja wa NSSF Frank Maduga alisema kuwa wao kama wafanyakazi wameamua
kujichanga na kuweza kusaidia hospitali hii kwa kuwapa vyandalua hii
ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria.
Alisema
kuwa mpaka sasa wameshatoa vyandarua 184 katika hospitali tofauti
ikiwemo ya Mount meru ,St Elizabeth,Levolosi pamoja na kwenye vituo vya
kulelea watoto yatima na wasiojiweza ambacho ni kituo cha walemavu Usa
river na hawataishi hapo tu wao kama wafanyakazi wamejipanga kila mwisho
wa mwezi kutoa msaada katika kila sehemu ambayo inamlenga mwananchi.
Alitoa
kwa wadau mbalimbali kujitoa kwa kuchangia na kusaidia kwa kutoa
misaada katika sehemu mbalimbali ikiwemo watoto yatima ,wasio jiweza na
hata katika hospitali zetu ili kuweza kuwapa moyo wahusika na sio
kusubiri tu serekali ifanye ,kwani kutoa ni moyo ivyo kila mtu anaeguswa
ajitokeze kutoa ikiwemo kuchangia wodi za hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment