Mkutano ulifanyika katika ofisi ya TIRDO ambayo ni Taasisi tanzu ya Wizara ya Viwanda na biashara, ambapo kulishuhudiwa utiwaji saini wa makubaliano kati ya GS1 Tanzania na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika kushirikiana kufanya kazi pamoja na kujenga mahusiano ambayo ni muhimu haswa kwa wazalishaji wa Tanzania kwani alama ya utambuzi wa bidhaa kwa sasa zinahitajika katika masoko yote ya ndani na nje ya nchi.
TBS imekua ikishirikiana na GS1 Tanzania katika uelimishaji wajasiliamali ambayo mafunzo kadhaa kati ya Taasisi hizi mbili yameshafanyika huko mkoani.
Wazalishaji wa Tanzania wanaotumia Barcode za nje ya nchi wanaaswa kubadilisha na kutumia Barcode(alama za uzalishaji) za hapa nchini kwani itasaidia:
- Kupunguza matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kulipia huduma hiyo.
- Kutupa takwimu rasmi za wazalishaji kwani kutumia barcode za nje ya nchi bidhaa inaonekana imetoka kwenye nchi nyingine na sio Tanzania.
- Kuwepo kwa utambulisho kwa bidhaa za Tanzania kwani nambari tatu za mwanzo za Barcode zinaonyesha bidhaa zinatoka nchi gani, ambapo kwa bidhaa za Tanzania utambulisho wetu ni 620.
- Mwisho ni suala zima la uzalendo, tujivunie cha kwetu.
Kuna wazalishaji wa Tanzania 13 tu ambao wamechukua alama za uzalishaji (barcode), sio tu wameonesha uzalendo bali wameendana na matakwa ya masoko yaliyo rasmi ya ndani na nje ya nchi. Huduma hii kama umekamilisha matakwa yote unaipata ndani ya siku moja tu.
GS1 Tanzania inahudumia nchi zaidi ya tano ambazo hazina huduma hii nazo ni Rwanda, Burundi, Uganda, Zambia, Malawi na Mozambique.
Mwenyekiti wa bodi GS1 Tanzania Dr. Gedion Mazara alifungua kikao kwa kuelezea kuhusu alama za utambulisho (barcode) na umuhimu wake.
Mkurugenzi mkuu wa GS1 Tanzania pia aliongelea ni jinsi gani wazalishaji wakipata na kutumia barcode/alama za uzalishaji itasaidia sana nchi
Mkurugenzi mkuu wa TBS(Shirika la viwango Tanzania) ,Mr. Joseph Masikitiko
Mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Uhamishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo
Wajumbe wa bodi ya GS1 Tanzania na wa TBS
Kuanzia kushoto Mkurugenzi mkuu wa TIRDO Prof. Madundo Mtambo, Mwenyekiti wa bodi GS1 Tanzania Dr. Gedion Mazara & Muwakilishi wa mgeni rasmi Odilo Mjengo
Baadhi ya wazalishaji waliofanikisha kuchukua alama za utambuzi wa bidhaa za barcode wakipokea membership license/certificate.
Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko Kilombero Sugar company
Shamim Mwasha aliwakilisha Lavy Beauty company limited ya mwanamitindo Flaviana Matata ambayo imepata Barcode ya Rangi zake za kucha za lavy Nail Polish.
Mkurugenzi wa GS1 Tanzania Fatma Kange akisaini mkataba na mkurugenzi wa TBS Joseph Masikitiko
Wakiwa wameshasaini mkataba.
Board Members wa GS1 katika picha ya pamoja
Board Members wa tbs
Wafanyakazi wa GS1 Tanzania
No comments:
Post a Comment