Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, DenisSebo akiwatambulisha watangazaji wapya wa kituo cha redio cha Efm,Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando kwa wananchi jana katika shindano la shika ndinga kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
Kituo cha EFM redio kwa mara nyingine tena kimeibuka na shindano lake la shika ndinga kwa mashabiki wake wa jiji la Dar na Pwani. Pamoja na kufanyika kwa shindano hilo lililozua msisimko mkubwa miongoni mwa wilaya ya Temeke,EFM Radiao pia waliwatangaza watangazaji wao Wapya watatu waliokuwa Clouds FM,Watangazaji hao ni Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando.
Shindano hilo Kwa mwaka huu ,limezinduliwa rasmi jana April 9/2016 kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar.
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo alisema kuwa shindano hilo litaendelea pia kwa wilaya ya Ilala, Kinondoni, Bagamoyo, na Kibaha na hatimae kilele chake kufanyika katika uwanja wa Sinza TP.
Sebo alisema kuwa Shindano hilo litaanza na washiriki 60 kwenye kila wilaya na washiriki 10 kati yao wanawake watano na wanaume watano ambao wataingia kwenye fainali ya kujinyakulia gari ambao wamepata nafasi ya kushiriki kwa njia ya kupiga simu na kujibu kiufasaha swali husika ili kupata nafasi ya kushiriki shindano la shika ndinga.
Alisema kuwa shindano hilo mwaka huu limeboreshwa zaidi kwa kutoa zawadi za pikipiki kwenye ngazi ya wilaya na magari kwenye ngazi ya fainali.
Lengo ni kuwawezesha wasikilizaji wake kwa namna moja ama nyingine katika kuongeza na kukuza kipato kitakacho changia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.

Watangazani wapya Paul James na Gerald Hando na ,Abel Onesmo akielekea jukwaani kutangazwa rasmi kwa wakazi wa Temeke,jijini Dar.
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, DenisSebo akishuhudia vijana wanavyoipakia ndinga katika gari kuelekea kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam
Ndinga na pikipiki zikiwa kwenye gari kuelekea kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam
Ndinga na pikipiki zikiwa juu ya jukwaa kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Shindano hilo wakiendelea kushindana kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Shindano hilo wakiendelea kushindana kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam
Watu wa huduma ya kwanza akimhudumia mshiriki wa Shindano hilo akiwa amezimia kutokana na mshtuko alioupata kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam
Watu wa huduma ya kwanza wakimhudumia mshiriki wa Shindano hilo akiwa amezimia kutokana na mshtuko alioupata kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam
Watu wa huduma ya kwanza wakimhudumia mshiriki wa Shindano hilo akiwa amezimia kutokana na mshtuko alioupata kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, DenisSebo (alie vaa tisheti nyeupe wa kwanza kushoto) akitiza Shindano hilo kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam
Mshindi wa shindano la shika ndinga alieshinda pikipiki Salehe Maga akizungumza na waandi wa habari (hawapo picha) juu ya kuushukuru uongozi wa Efm kwa kuanzaisha shindano hilo.
Mshindi wa shindano la shika ndinga alieshinda pikipiki Philipina Mshanga akizungumza na waandi wa habari (hawapo picha) juu ya kuushukuru uongozi wa Efm kwa kuanzaisha shindano hilo , na kuwaomba wakina wanawake wajitokeze kwa wingi kwenye mashindano hayo.
Wananchi wakifatilia mashindano hayo (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).
No comments:
Post a Comment