Thursday, April 7, 2016

DKT. SHEIN AWAONGOZA VIONGOZI MBALIMBALI KATIKA DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU MZEE KARUME

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mara alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuika na Viongozi na wananchi katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi wa Mjini na Mashamba waliojumika kwa pamoja katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi kwa pamoja wakiwa katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Miongoni mwa Akinamama wakimuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume wakati wa Hitma iliyosomwa leo katika Osifi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Wananchi mbali mbali wa dini tofauti.
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwana Mwema Shein (katikati) Mama Fatma Karume (wa pili kulia) pamoja na Wake wa Viongozi wakiwa katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Wanafunzi wa Madrasa kutoka Vyuo mbali mbali na wananchi waliohudhuria katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe,Amani Abeid Karume,(wa pili kushoto) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Ali Hassan Mwinyi(wa pili kulia) Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania Mhe.Mohammed Gharib Bilali(kulia)kwa pamoja wakiitikia dua iliyoombwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheik Khamis Haji Khamis baada ya kumalizika kisomo cha Hitma ya dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Sheikh Hamid Masoud Jongo kutoka Jijini Dar es Salaam akitoa mawaidha baada ya Hitma ya dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,kuweka Shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China Bwana Xie Yunliang akiwawakilisha Mabalozi wa Nchi mbali mbali katika kuweka shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Mjukuu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Ahmed Amani Abeid Karume akichukua shada la mauwa kwaniaba ya wenzake kuliweka katika kaburi baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea Marehemu Babu yao, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,(wa pili kulia) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanawema Shein (kushoto) Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume,Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi pamoja wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akifuatana na wasaidizi wake akitoka eneo la kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume liliopo nje ya Jengo la Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar baada ya kumalizika hafla ya dua na uwekaji wa mashada ya mauwa iliyofanyika leo,na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono viongozi na wananchi walihudhuria katika hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo baada ya kumalizika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar na uwekaji wa mashada ya mauwa ambapo Viongozi na Wananchi mbali mbali walihudhuria
Wake wa Viongozi wakiwa nje ya Ofisi Kuu wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar baada ya kumalizika kwa hitma ya kumuombea dua Rais wa kwaanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeeid Amani Karume iliyofanyika leo. [Picha na Ikulu.]

No comments: