Saturday, April 30, 2016

ACACIA ILIYOSHIRIKI MAONYESHO YA MEI MOSI MJINI DODOMA

Baadhi ya watu wakiwa katika banda la Kampuni ya kuchimba madini ya ACACIA Bulyanhulu wakati wa maonyesho ya sherehe za Mei Mosi kitaifa mjini Dodoma, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA).
  Ofisa Afya na Usalama mahali pa kazi kutoka kampuni ya kuchimba madini ya Acacia Bulyanhulu, Michael Nota (kushoto) akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa ya usalama kwa watu waliofika katika banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya sherehe za mei mosi kitaifa mjini Dodoma jana, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakaz Tanzania (TUCTA).  
Watu wakitoa maoni yao walipofika katika banda la ACACIA 
 Ofisa Afya na Usalama mahali pa kazi kutoka kampuni ya kuchimba madini ya Acacia, Michael Nota akionyesha ramani inayoonyesha maeneo yanayopatikana madini.
 Baadhi ya watu wakipimwa HIV walipofika katika banda la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Emergency Purpose Officer wa GGM,  Mwaimu Mohamed (kulia) akionyesha vifaa vya kutoa huduma ya kwanza. 
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Umonga iliyopo Dodoma wakiangalia mfano wa meli ya mizigo walipotembelea banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
 Mkurugenzi wa Zimamoto na Usalama Bandari ya Dar es Salaam (PTA), Dunstan Biyego akionyesha moja ya vifaa vya uokoaji cha zimamoto bandarini.
Bw. Abdul Masoud wa Bandari ya Dar es salaam akionyesha viatu maalumu vinavyotumiwa na wazamiaji kuogelea.

No comments: