Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini wakati alipowasili katika
kambi ya Rumasi-Lukole iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera,kambi hiyo hutumika kupokea
wakimbizi wanaotoka nchini Burundi ambapo baadae hupelekwa katika makambi ya Nyarugusu
yaliyopo mkoani Kigoma.Waziri Mkuu yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
Kikundi cha ngoma za kitamaduni cha Umoja, wakicheza ngoma wakati Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa alipowasili katika kambi ya Rumasi-Lukole iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera,
kambi hiyo hutumika kupokea wakimbizi wanaotoka nchini Burundi ambapo baadae hupelekwa
katika makambi ya Nyarugusu yaliyopo mkoani Kigoma.Waziri Mkuu yupo mkoani Kagera kwa
ziara ya kikazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi,iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi,Harrison Mseke, akisoma taarifa ya kambi ya Rumasi-Lukole mbele ya Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu kambini hapo kukagua kambi hiyo na
kuongea na raia wa Tanzania na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambini hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza
na wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo pichani),wakati ya ziara
aliyoongozana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.Kambi hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani
Kagera hupokea wakimbizi kutoka nchi ya Burundi kabla ya kuwapeleka kwenye makambi ya
wakimbizi ya Nyarugusu,mkoani Kigoma.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,akizungumza na raia wa Tanzania pamoja na wakimbizi wa
Burundi wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo pichani), Waziri Mkuu alitembelea
kambi hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera na kuwaasa wakimbizi hao kuishi kwa
kufuata sheria za nchi pasipo kuvunja amani iliyopo nchini.
Raia wa Tanzania pamoja na wakimbizi kutoka nchi ya Burundi, wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa(hayupo pichani),wakati wa mkutano aliozungumza nao katika kambi ya
wakimbizi ya Rumasi-Lukole,iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kigoma.
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa(wa tatu kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya
Huduma za Wakimbizi,iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Harrison Mseke
(wapili kulia),wakati akielekea kukagua mabweni wanayolala wakimbizi kutoka Burundi katika
kambi ya Rumasi-Lukole,iliyoko wilayani Ngara,mkoani Kagera.Wa kwanza kushoto ni Naibu
Waziri wa Nishati na Madini,Dk.Medard Kalemani , wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni mwakilishi wa
Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani(UNHCR),Gerald Ndabimala.
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa,akikagua mabweni wanayolala wakimbizi kutoka nchini
Burundi katika kambi ya Rumasi-Lukole inayotumika kupokelea wakimbizi hao.Kambi hiyo iko
wilayani Ngara,mkoani Kagera.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za
Wakimbizi,iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Harrison Mseke.(Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment