Naibu waziri wa maji na umwagiliaji mhandisi Izack Kamwele akikagua chanzo kikuu cha maji safi na salama cha mradi wa kuongeza upatikanaji wa maji katika mji wa kigoma kilichopo eneo la katonga.
Baadhi ya vibarua katika mradi huo wakifukia mabomba ya kupitisha maji yanayotoka kwenye chanzo katika eneo la Katonga
Naibu waziri na Mhandisi Izack Kamwela akiongea na waandishi baada ya kukagua mradi wa maji Kigoma
Na, Editha Karlo,wa blog ya jamii Kigoma
NAIBU Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwela amewabana wakandarasi wa mradi wa maji wa kuongeza uwezo wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa Mkoa wa Kigoma kwa kushindwa kumaliza mradi kwa muda muafaka uliokuwa ndani ya mkataba.
Akiongea na wakandarasi hao katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa kayika kwenye ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea mradi huo alisema kuwa mradi huo ulitakiwa kuisha mwaka jana mwezi wa kumi na mbili laki mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 46 tu.
"Huu mradi ulitakiwa uishe ndani ya miezi 24 kwa mujibu wa mkataba lakini sasa hivi ni miezi 34 mpo nje ya mkataba nataka kujua tatizo ni nini? hii siyo kasi ya awamu ya tano"Alisema Mhandisi Kamwele.
Aliongeza kwa kusema kuwa sasa hivi kila wiki mkandarasi anatakiwa kukaguliwa na akishindwa kukamilisha kazi mkataba wake utavunjwa, na kama hawezi kukamilisha kazi kwa wakati atafute wakandarasi wenzake wamsaidie tena wakandarasi hao wawe daraja la kwanza.
Alisema kuwa mradi huo unatakiwa kukamilika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu na usipo kamilika wahusika watawajibishwa kwani watakuwa wameipatia serekali hasara kubwa.
Naye Mhandisi mshauri wa mradi huo Michael Mwamkinga alisema kuwa mradi huo ulitakiwa uwe umekamilika march 2015 lakini mpaka sasa ni asilimia 46 tu za mradi huo ndo zimekamilika.
Alisema sababu zilizopelekea mradi huo kushindwa kukamilila kwa wakati ni mkandarasi aliyepewa tenda hiyo ambaye ni SPEECON alikopa fedha kutoka Equity Bank na kushindwa kulipa mkopo huo atimaye bank imeamua kumfirisi.
Mwamkinga alisema kuwa mpaka sasa asilimia 98 za mradi huo upo chini ya bank hiyo ambapo mradi huo unagharimu zaidi ya euro bilioni 16 chini ya ufadhiri wa European union(umoja wa nchi za ulaya).
Alisema kuwa baada ya miezi miwili mradi huo utakuwa umekamilika kwa asilimia 70.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya alisema kuwa hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika mji wa Kigoma umeongezeka kutoka asilimia 56 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 68 mpaka sasa kwasababu ya mradi wa uboreshaji wa maji safi na salama vijijini.
Machibya alisema kuwa changamoto ziluzopo Kigoma katika sekta ya maji ni upotevu wa maji,ukosefu wa mitambo ya kusafirishia maji, upungufu wa wataalam wa maji kwa Wilaya zote na ukosefu wa pesa za kuboreshea miradi ya maji vijijini.
No comments:
Post a Comment