Na Dixon
Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .
VYOMBO vya ulinzi
na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa
kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu, raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati
ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini Armenia.
Wanyama hao wakiwa
kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia wanyama walikuwa wasafirishwe kwa
ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa nchini Belarus
kupitia kampuni ya Arusha Freight Limited ya jijini Arusha.
Raia hao wa
Uholanzi waliokamatwa juzi majira ya saa 1:30 jioni katika uwanja wa ndege wa KIA
wametambulika majina yao kuwa ni Arten Vardanian (52) aliyekuwa na hati ya
kusafiria yenye namba NWF8CKJR8 na
Edward Vardanian (46) aliyekuwa na hati ya kusafiria namba NY969P96.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa akiwa ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari.
Meneja usalama
uwanja wa ndege KIA,Kisusi Justine aliliambia Tanzania Daima mbali na kukamatwa
kwa raia hao wa kigeni pia walifanikiwa kumshikilia Mtanzania ,Idd Misanya
anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.
“Wahusika hawa
wawili walifika eneo la Cargo ambako walikuwa katika harakati za kusafirisha
wanyama hao ndipo tulipowashikilia kwa sababu taratibu za kusafirisha wanyama
Hai zilikiukwa”alisema Justine.
Kuhusu mazingira
ya kukamtwa kwa watuhumiwa hao ,Justine alisema ndege hiyo inaonekana ilitua
katika uwanja huo mahususi kwa ajili ya kubebeba wanyama hao na kwamba ili
ruhusiwa kuondoka jioni ile baada ya kukamatwa kwao.
Kamnda wa Polisi
mkoa wa Kilimanjaro Kamishna msaidizi wa Polisi ,Wilbroad Mutafungwa
alithibitisha kukamatwa kwa raia hao na kwamba wamehifadhiwa katika kituo cha
Polisi cha KIA huku uchunguzi zaidi ya tukio hilo ukiendelea.
“Mnamo Machi 23
mwaka huu majira ya saa 1:30 jioni huko uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA ) tulifanikiwa kuwakamata raia wawili wa Uholanzi wakiwa
wanataka kusafirisha wanyama aina ya tumbili na tayari uchunguzi kwa kushirikiana
na Wizara ya maliasili na Utalii unaendelea”alisema Mutafungwa.
Kamanda Mutafungwa
alisema taarifa za awali zinasema wanyama hao waalisafirishwa hadi uwanjani
hapo wakitokea mpakani mwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo kampuni ya
uwakala ya Arusha Fright Limited ilipewa kazi hiyo.
Alisema uchunguzi
wa awali unaonesha ndege ya mizigo iliyokuwa isafirishe wanyama hao ni ya
binafsi huku akikanusha kukamatwa kwa mtu mwingine anyetajwa kuhusika katika
kuuza wanyama hao kwa raia hao wa Uholanzi.
“Mpaka sasa
tumewakamata hao raia wawili ,lakini kama nilivyosema uchunguzi unaendelea
tukishirikiana na wizara ya maliasili na utalii ili tuone kama kuna washiriki
wengine wa tukio hilo ,so far tunao hao wawili tu”alisema Mutafungwa.
Alisema mbali na
hati za raia hao wa uholanzi kuonesha
kuwa walikuwa wakiishi nchi kihalali bado vyomb vya ulinzi na usalama ikiwemo
idara ya Uhamiaji vimeanza kuchunguza pia uhalali wa vibali vya raia hao vya
kuishi nchini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment