Monday, March 7, 2016

TAASISI YA BENJAMIN MKAPA KUADHIMISHA MIAKA KUMI.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Foundation, Dk. Ellen Mkondya Senkoro akiongea na waandishi wa habari kutangaza maadhimisho ya miaka kumi ya taasisi hiyo pamoja na shughuli mbalimbali zitazoambatana na maadhimisho hayo jijini Dar es salaam jana. Taasisi hiyo imekuwa kinara katika kuongoza jitihada za kuimarisha utoaji huduma za afya nchini katika miaka kumi iliyopita. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Programu za Taasisi hiyo Raheli Sheiza.
Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF) imeendelea kutekeleza kutekeleza jitihada za serikali ya Tanzania na washirika wake katika kuimarisha utoaji huduma za afya katika maeneo yasiyopata huduma ya uhakika na mwezi Aprili 2016, itaadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa Aprili 2006 na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniania, Mhe. Benjamin William Mkapa. 

 Afisa Mtendaji Mkuu wa BMF, Dk. Ellen Mkondya-Senkoro amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari leo , kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya miaka kumi ni “Miaka 10 – Tumejituma, Tumeaminika na Tumeweza”. 

Taasisi ina furahia kuweza kubadilisha maisha na afya za mamilioni ya Watanzania ambao wamefikiwa moja kwa moja na ambao hawakufikiwa moja kwa moja ya Taasisi.

 Ameongeza kwamba “Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo, Taasisi ya Benjamin Mkapa itafanya shughuli mbalimbali za kijamii kuanzia March 2016 hadi mwisho wa Aprili 2016. 

Shughuli hizo ni pamoja na utoaji huduma za afya kwa jamii, kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yamekuwa yakihudumiwa na taasisi, mkutano wa wadau, na chakula cha usiku kuchangisha fedha. 

Katika kipidi hiki tutawatambua na kuwapa tuzo watu mbalimbali na taasisi ambazo zimechangia ukuaji na mafanikio ya taasisi. Dk. Ellen alisema “Bodi ya Wadhamini ya BMF, Wafanyakazi pamoja na familia zao watachangia damu kwenye.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa nia mojawapo kuwasaidia watoto wenye maradhi, akina mama wajawazito na wagonjwa wanaohitaji damu ili kuweza kupona.

 Pia tutatoa elimu, ushauri nasaha na kuwapima VVU wagonjwa ambao wao kwenye vituo vya afya vya umma kwenye mikoa ya Rukwa na Simiyu. Elimu ya afya kuhusiana na Ukimwi na afya ya uzazi pia vitatolewa kwenye shule mbili kaika mikoa hiyo”. 

 Katika miaka kumi, taasisi ina fahari kuweza kubuni mbinu endelevu za kutatua changamoto za kitaifa kwenye sekta ya afya “Tunaona fahari kuweza kutoa ajira kwa zaidi ya watoa huduma za afya 1,100 ambao wamehudumia maeneo yenye uhitaji mkubwa, kutoa nafasi za masomo kwa wanafunzi 1,000 wanaosoma kozi za elimu ya afya na kuweza kuwapa motisha watumishi wa sekta ya afya kwa kuwajengea nyumba 480 za kuishi katika vituo vya afya vijijini. Taasisi pia imeweza kuwafikia watumishi wa huduma ya afya zaidi ya 800 na kuwapa mafunzo kuhusu utoaji huduma bora za afya kuhusu ukimwi na afya ya uzazi”, alisema Dk. Mkondya-Senkoro. 

 Uchangishaji fedha tayari unaendelea ambapo makampuni mbalimbali yameonyesha nia, mengine yametoa ahadi na kutoa fedha pamoja na mali na makampuni hayo ni pamoja na Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Bank M, Clouds Media Group na wengine. Tunatarajia kupata ahadi zaidi kupitia hafla maalum ya chakula cha jioni shughuli ambayo itahudhuriwa na wageni waalikwa 150.

 Katika hafla hiyo Taasisi ya Benjamin Mkapa imelenga kuchangisha shilingi bilioni moja ikiwa ni sehemu ya bajeti yake ya mwaka wa Fedha hizo zitawanufaisha Watanzania kupitia uimarishwaji wa nguvu kazi katika sekta ya afya na huduma nyingine za afya hususani kwenye ukimwi, uzazi, na afya mama na mtoto. Vile vile, taasisi itaitumia hafla hiyo kuzindua jina lake jipya litakalojulikana kama “ “Benjamin W. Mkapa Foundation” na kuondokana na “ Benjamin W. Mkapa HIV/AIDS Foundation”. Dr. Mkondya-Senkoro aliongeza: “Katika jitihada zetu kuwa endelevu, kuongeza ukuaji, ili kuendana na mazingira yanayobadilika kitaifa na kimataifa ikiwemo maendeleo ya sekta ya afya, kuanzia tarehe 2 Novemba 2015, tumebadilisha jina letu kuwa “The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF)”. 

Mabadiliko haya ni kutokana na lengo la taasisi kupanua wigo na kutekeleza programu katika maeneo mengi zaidi ya ukimwi. Malengo makuu ya taasisi hii yatabakia vilevile ikiwa ni kuwaletea matumaini Watanzania waishio mazingira duni”.

No comments: