Friday, March 25, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Watanzania watahadharishwa kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu kufuatia baadhi wagonjwa kushindwa kumaliza dozi na kupelekea maabukizi na kupelekea wagonjwa sugu. https://youtu.be/_amYeDO-0EM  

Baadhi ya wakazi wilayani Mkuranga mkoani Pwani wailalamikia kampuni ya umeme ya TANESCO kutokana na mpango wake wa kutaka kupitisha miundombinu ya umeme katika mashamba yao bila ya kuwapatia fidia. https://youtu.be/HVn6YJalJtE  

Kufuatia mabadiliko ya tabia ya nchi yanayopelea uwepo wa ukame nchini baadhi ya wananchi wa Lorya waiomba serikali kuwatafutia njia mbadala ya kilimo ili kuwaepusha na baa la njaa. https://youtu.be/b7iu98v8z0Q  

Wakala wa usambazaji wa pembejeo za kilimo za ruzuku wakamatwa na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuwalaghai wakulima. https://youtu.be/HjdT4SZ7AAk  

Zaidi ya wanafunzi elfu 5 walioandikishwa darasa la kwaza wilayani Geita wanalazimika kusomea chini ya miti kufuatia uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa kutokana na uandikishaji kuwa mkubwa. https://youtu.be/fHZ-Q34wza4  

 Waumini wa dini ya kikristo kote nchini waemeungana na wenzao duniani kote katika kuadhimisha mateso na kifo mwokozi wao Yesu Kristo; https://youtu.be/LzGFknPICPU  

Mkuu wa wilaya Lorya mkoani Mara atangaza mpango wa kuanza operesheni ya kupambana na uharamia ndani ya ziwa victoria ili kukomesha vitendo vya uhalifu dhidi ya wavuvi na mali zao. https://youtu.be/0r1mzOlA_Qc  

Jeshi la polisi Mkoani Manyara latoa siku 60 kwa wamiliki wa silaha mkoani humo kuhakiki na kusalimisha silaha zao kabla ya msako mkali kuwakumba.https://youtu.be/k695fRMUXf8  

Baadhi ya wakazi wa Sinza Tandare jijini Dar es salaam wameliomba shirika la maji safi na maji taka jijini humo DAWASCO kuwaunganishia maji kuondokana na kero mbalimbali wanazozipata katika kupata huduma hiyo. https://youtu.be/AOrbzc8ldD8  

Rais John Magufuli atoa zawadi ya siku kuu ya pasaka kwa kambi ya wazee ya NJoro na kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira hatari cha Upendo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro. https://youtu.be/PJH4ch1VKig

No comments: