Kwa mara ya kwanza, wadau wa Sanaa nchini wamepata fursa ya kukutana
na Makampuni, Mashirika na Vyombo mbalimbali katika mafunzo
yaliyofanyika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. Semina hii
iliongozwa na Maria Sarungi Tsehai, ambaye ni mdau mkubwa katika sekta
hii
Mafunzo hayo yalifanywa na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama
Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba, Arden Kitomari,akitoa
mafunzo ya namna ya kuwekeza katika Sekta ya Nyumba nchini
Tanzania,hususan kupitia miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa
Wadau wa Sanaa pia walipata mafuzo ya Namna ya kubalansi maisha yao ya
Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt
Sadaka Gandi.
Semina hii iliyopewa jina Celebrity Corporate Conference &
Cocktail iliwahusisha pia COSOTA na BASATA ambao ni wasimamizi wakuu
wa kazi za sanaa na taratibu zake
Ms Doreen Anthony Sinare, CEO wa COSOTA akitoa somo kuhusu usajili wa
kazi, masharti ya kuzingatiwa na Sheria zinazomlinda Msanii
aliyesajiliwa
Sekta lengwa katika semina hii ni wadau kutoka Filamu, Muziki, Urembo,
Habari, na Wajasiriamali mashughuri
Bwana Aristides kutoka BASATA aliwaelekeza wadau kuhusu Taratibu mpya
za kujisajili na chombo hiki, pamoja na faida zake.
Je, Unafahamu namna ya kuifanya Talanta yako kuwa Biashara? Hii ndio
ilikuwa mada iliyoongozwa na Mjasiriamali mashughuri, Shekha Nasser wa
Shear Illusions
Baada ya mada zote kukamilika, wadau walipata fursa ya kubadilishana
mawazo na kujadili walichojifunza, kwa kushiriki Tafrija mchapalo
iliyoandaliwa
Huu ukawa wakati muafaka wa wasanii kuuliza maswali na kutoa dukuduku
zao kwa Makampuni, Mashirika na vyombo vinavyohusika na Sanaa na
Wasanii. Mrembo na Mjasiriamali Jokate Mwegelo akiteta jambo na afisa
kutoka BASATA
Mwanahabari Maimuna Kubegeya hakuwa nyuma kuuliza maswali na
kufahamiana na CEO wa COSOTA, Ms Doreen Anthony Sinare
MwanaBlog maarufu John Bukuku akifurahia jambo na Meneja Masoko wa
NHC, Arden Kitomari
Antu Mandoza akisisitiza jambo
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Popular Links ambao ndio waandaaji
wa Semina hii akiwa katika pozi na Mkurugenzi Ruge Mutahaba kutoka
Clouds Media
Warembo katika picha ya pamoja
Wasanii wa kutengeneza muonekano kutoka LuvTouch Manjano ya Shear
Illusions, wakiwaonesha baadhi ya wageni, namna ya kupaka makeup
Mariam Ndabagenga, Mkurugenzi wa Popular Links akitoa neno la Shukran
kwa wageni waalikwa wote na kuwakaribisha kwenye awamu ya pili ya
Semina hii itakayofanyika mwezi Oktoba.
Semina hii ya Celebrity Corporate Conference & Cocktail
imeandaliwa na Kampuni ya Popular Links kwa udhamini wa Heineken, The
Guardian, Nipashe, Leteraha, Hyatt Regency hotel, Ndovu Special Malt,
Cocacola, NHC, COSOTA, Jamii Media, BASATA, Shear Illusions, Clouds
Media na Slide Visuals.
No comments:
Post a Comment