Tuesday, March 15, 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA MIKOA, MKURUGENZI WA TAKUKURU NA KAMISHNA MKUU WA TRA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Said Meck Sadiki kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Rehema Nchimbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Said Thabit Mwambungu  kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Magesa Mulongo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Amina Juma Masenza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa leo Ikulu jijini Dar es salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Halima Omary Dendegu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Jordan Mungire Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven  kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Paul Makonda  kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga  kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Ikulu jijini Dar es salaam leo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga  kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Alphayo Kidata kuwa  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakiimba wimbo wa Taifa kabala ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Wakuu wa Mikoa wapya wa Tanzania Bara walioapishwa leo wakiwa katika picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es salaam.
 Wakuu wa Mikoa wapya walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila kiapo cha kuzingatia maadili ya viongozi wa umma katika kutekeleza majukumu yao leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa wapya walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakisaini hati za viapo vya maadili ya viongozi wa umma mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.Picha/Eleuteri Mangi na Aron Msigwa.

Na Jacquiline Mrisho- Dar es salaam.     

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapa siku 15 Wakuu wa Mikoa kuwaondoa watumishi hewa walio katika orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi wa umma katika Mikoa yao.

Rais Dkt. Magufuli amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa aliowateua Machi 13 mwaka huu ambapo amewaagiza washirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri kuwaondoa watumishi hewa.

“Nimewapa siku 15 kuanzia leo mkashirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri zenu kuwatoa wafanyakazi hewa, nikigundua kuwa bado kuna wafanyakazi hewa, Mkurugenzi husika atafukuzwa kazi na atapelekwa mahakamani”,

Na kusisitiza “Nimeamua kuwachagua nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika Mikoa yenu, nawaomba mkatimize majukumu yenu bila kuogopa” alisema Dkt. Magufuli.

Aidha, Mhe.  Dkt. Magufuli amesikitishwa na utafiti wa watumishi uliofanywa katika Mikoa ya Singida na Dodoma ambapo imegundulika watumishi 202 wanalipwa mishahara hewa.

Wakati wa utafiti huo, zaidi  ya watumishi 26,900 walioko katika Halmashauri 14 za Mikoa hiyo, watumishi 3,320 hawakuwepo kazini kwa sababu mbalimbali.

Kwa mantiki hiyo, ukichukua utafiti huo wa Mikoa miwili ni dhahiri Serikali inapoteza mapato mengi kwa kulipa mishahara ya watumishi hewa nchi nzima.

Vivyo hivyo, Mhe. Dkt. Magufuli amewasisitiza Wakuu wote wa Mikoa wakasimamie ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa waliahidi kutatua kero za wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani ya nchi yao.

Naye Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri zote nchini wajiandae kupokea na kuzipangia matumizi shilingi milioni 50 za kila Kijiji zilizoahidiwa wakati wa kampeni kwa lengo la kuboresha na kuimarisha shughuli za maendeleo.

No comments: