Friday, March 11, 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY ATEMBELEA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA



Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Masika(kushoto)akimwongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kuwasilimia wafanyakazi wa taasisi hiyo katika ziara yake ,Norway ni moja ya nchi zinazosaidia sekta ya elimu ya ufundi nchini. 

Ujumbe uliongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kutoka Norway na maafisa kutoka ubalozi wao nchini wakisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen (kulia)akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen na ujumbe wake wakipata maelezo ya mfano wa kuzalisha umeme unaotokana na chanzo kidogo cha maji. 
Mmoja wa wanafunzi anayesoma katika Chuo hicho akimpa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen maelezo kuhusiana na kozi yake. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo.Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

No comments: