Wednesday, March 30, 2016

MWANZA NA ARUSHA YAONGOZA WATUMISHI HEWA.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.


MKOA Mwanza waongoza kuwa na watumishi  hewa 334  ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kwa kuwa na watumishi hewa 270 ikiwa nchi nzima na watumishi  hewa 2,702.

Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyo kuwa na watumishi hewa kukosekana kwa watumishi hewa katika mkoa wa shinyanya imetokana na mikakati ya mikoa hiyo kila idara kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa mishahara kila mwezi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Killango kuwa viongozi walioanza katika mikoa huo walijipanga katika kuondokana na watumishi hewa.
Mkoa wa Songwe kukosekana kwa watumishi hewa kunatokana na upya wake na mkuu wake mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita.

Akizungumza na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa miradi ya kuongeza mapato.

Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa kuondokana na matumizi yasio na ulazima ili fedha hizo zitumike katika matumizi ya msingi.

Amesema kuwa zoezi hilo liweze kuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kushughulika na watoro ambao wanalipwa fedha wakati hawafanyi kazi,
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema wote ambao wamehusika na hujuma za mishahara wafikishwe katika vyombo vya dola na mkoa wake umeanza kutekeleza.
 Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi majina hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik  akikabidhi majina hewa kwa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene  baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa , jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa Mikoa na Watendaji wa TAMISEMI wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

No comments: