Thursday, March 3, 2016

MFUKO WA HIARI WA PSPF WANUFAISHA MAMIA YA WAKAZI WA UKONGA

Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard akizungumza na wananchi wa Ukonga pamoja na maeneo mengine ya mji wa Dar es Salaam kuhusu Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa Semina ya Ujasiriamali Ukonga jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard akifafanua jambo kwa wajasiriamali kuhusu Mfuko wa Hiari wa PSPF jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mjasiriamali kwanza Enterprises Dr. Didas Lunyungu.
Wajasiriamali kutoka maeneo ya Ukonga na maeneo mengine ya mji wa Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini elimu iliyokuwa ikitolewa kuhusu uchangiaji wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa semina ya wajasiriamali jana jijini Dar es Salaam
Afisa Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe akitoa elimu kwa wachangiaji wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa kuandikisha wachangiaji wapya wa mfuko huo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe akitoa elimu kwa wachangiaji wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa kuandikisha wachangiaji wapya wa mfuko huo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Mrisho Ngongo (kulia) akitoa fomu za kujisajiri kwa wachangiaji wapya wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF jana jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanachama wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakiwa katika mstari kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho za kujisajiri katika mfuko huo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe (kushoto) akikagua fomu za uanachama wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF baada ya kusajili wanachama wapya jana jijini Dar es Salaam.Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
…………………………..

Na: Genofeva Matemu – Maelezo


Wananchi zaidi ya 500 kutoka zoni ya ukonga jijini Dar es Salaam wamejitokeza na kujisajiri kuwa wanachama wa hiari katika mfuko wa hiari wa PSPF ili kuweza kunufaika na mafao yatolewayo na mfuko huo.

Wananchi hao walipata fursa ya kujisajiri wakati wa semina ya ujasiriamali iliyofanyika siku ya jana maeneo ya Ukonga jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na wananchi wapatao 1600 kutoka zoni ya Ukonga na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Akizungumza wakati wa semina hiyo Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Delphin Richard amesema kuwa mfuko wa hiari wa PSPF uliundwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuwa na akiba ya ziada kwa kutoa uhuru kwa mwanachama kuchangia kwa kutegemea upatikanaji wa kipato cha ziada kitakachomwezesha kujiwekea akiba.

Bw. Richard amesema kuwa lengo la PSPF ni kushiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii ili kuweza kutoa elimu ya mfuko wa hiari wa PSPF hivyo kutoa nafasi kwa wajasiriamali, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, na watu binafsi kuchangia katika mfuko wa hiari kipato chao cha ziada kwa ajili ya akiba ya ziada.

Kwa upande wake Afisa Masoko Bibi. Sarah Adebe amesema kuwa jamii imekua na muitikio mkubwa wa kujisajiri katika mfuko wa hiari wa PSPF kwani mfuko huo unatoa huduma kwa kuchangia gharama ndogo hivyo kuwanufaisha wanachama hasa wa kipato cha chini.

Naye Mjasiriamali kutoka zoni ya Ukonga Bi. Doris Kimaro amesema kuwa ujio wa elimu ya mfuko wa hiari wa PSPF ni mafanikio makubwa katika familia yake kwani atatumia nafasi aliyoipata kwa kuchangia kipato chake cha ziada ili aweze kunufaika na fao la elimu litakalomuwezesha kukidhi mahitaji yake ya baadae.

Mfuko wa hiari wa PSPF umelenga kusaidia jamii kwa kuwa na mafao saba ambayo ni fao la elimu, fao la ujasiriamali, fao la uzeeni, fao la kifo, fao la ugonjwa/ulemavu, fao la kujitoa na fao la matibabu.

No comments: