MABONDIA PIUS KAZAULA WA PILI KUSHOTO AKIWA NA MPINZANI WAKE SEBA TEMBA |
REFARII WA MPAMBANO WA MASUMBWI SAID CHAKU AKIWAINUA MIKONO JUU MAONDIA PIUS KAZAULA KUSHOTO NA SEBA TEMBA BAADA YA MPAMBANO WAO KUMALIZIKA KWA DROO |
Bondia mohamed Matumla kushoto akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa mpambano uho ulisha kwa droo
Mabondia Mada Maugo kioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdallah Pazi wakai wa mpambano wao Pazi alishinda kwa T.K.O ya raundi ya tatu wakati wa mpambano wao uliofanyika uwanja wa ndani wa Taifa
Mabondia Nassibu Ramadhani kushoto akionshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa raundi nane uliofanyika katika uwanja wa ndani wa taifa siku ya jumapili ya psaka mpambano uho ulisha kwa maamuzi ya droo
Bondia Pus Kazaula kushoto akimrushia kunde la mkono wa kushoto mpinzani wake Seba Temba wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili ya pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam mpambano uho walitoka droo
------------------------------
MASHABIKI wapata burudani mashabiki waliofika uwanja wa ndani wa taifa kulikokuwa kunafanyika mchezo wa masumbwi wametoka na furaha tele baada ya kushuhudia mapambano waliyokuwa wakiyasubili kwa hamu kubwa hapa nchini.
Akizungumza baada ya kumalizika mpambano uho mratibu wa mapambano hayo Rajabu Mhamili 'Super D' amesema mashabiki wamefurahia mapambano ambayo karibia yote yalimalizika kwa droo
Akitaja matokeo ya mapambano hayo amesema bondia Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe' alimsambaratisha bondia Mada Maugo kwa T.K.O ya raundi ya tatu wakati Mohamedi Matumla na Cosmas Cheka waritoka droo wakati Pius Kazaula alitoa Droo na Seba Temba.
Mpambano mwingine mkali uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi nchini. Kati ya bondia Nassibu Ramadhani na Francis Miyeyusho nao pia umemalizika kwa sare.
Wakati huo huo mabondia Mfaume Mfaume na Ramadhani Shauri wanatarajia kusaini mkataba wa kuzipiga siku y mei mosi katika uwanja huo huo wa taifa
No comments:
Post a Comment