Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kilosa wakati alipokuwa
akiongea nao walipotembelea shule ya palakuyo kutoa vifaa vya kusomea masomo ya Sayansi na
kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina
ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa.maafisa hao walitoa pia msaada wa vifaa vya kusomea masomo
ya sayansi.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.sylvia Lupembe(kushoto)
akikabidhi vifaa vya kusomea masomo ya sayansi kwa mkuu wa wilaya ya kilosa Bw.John Henjewele
wakati wakati wa kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akigawa msaada wa vitabu
kwa watoto wa shule ya Mabwerebwere wilayani kilosa wakati walipotembelea walayani hapo kusaidia
masuala ya elimu pamoja na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na
wafugaji.
Mkurugenzi Idara ya Habari- MAELEZO Bw.Assa Mwambene(wa tatu kushoto) akikabidhi madawati
kwa watoto wa shule ya msingi Tindiga wakati maafisa habari na mawasiliano wa serikali
walipotembelea shule hiyo kugawa madawati na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina
ya wakulima na wafugaji wilayani kilosa.Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya kilosa Bw.John
Henjewele(wa pili kulia).
Picha na Daudi Manongi.
No comments:
Post a Comment