Wednesday, March 16, 2016

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA), LEO ASUBUHI KUJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI ZINZOFANYWA NA MAMLAK HIYO

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Aloyce Matei, akitoa ufafanuzi wa gati zilizo katika bandari hiyo kuhusu kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Aloyce Matei, akitoa ufafanuzi kuhusu namna Kamera zinazoendelea kufungwa katika Bandari hiyo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, waliotembelea Mamlaka hiyo leo Asubuhi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Aloyce Matei, akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu eneo itakapojengwa gati ya 13 na 14.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Mizigo Bandarini (TICTS), Paul Wallace akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu namna kampuni hiyo inavyohudumia makontena katika bandari ya Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sehemu ya Uchukuzi, Dkt. Leornard Chamuriho akitoa taarifa ya namna Wizara inavyosimamia Mamlaka zilizo chini yake,wakati Kamati ya Bunge ya MIundombinu, ilipotembelea Mamlaka ya Bandari(TPA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Aloyce Matei, akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu.

No comments: