Sunday, March 13, 2016

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Simu.tv: Viroba bandia vyenye gongo zaidi ya elfu tatu na mianane pamoja na bidhaa mbalimbali zenye uzito wa tani na nusu vyatekezwa wilayani Rombo baada ya kuingizwa wilayani humo kinyemela kupitia njia za panya. https://youtu.be/XHf3ZxxRYjM

Simu.tv: Shirika la maji safi na maji taka mkoani Dar es salaam DAWASCO, lawataka wamiliki wa majengo marefu mkoani humo kuepuka kujiunganishia maji ya shirika hilo kwani atakaye bainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria. https://youtu.be/6AzK9WGe7z0

Simu.tv: Viongozi wa dini mbalimbali visiwani Zanzibar wakutana kujadili namna ya kuendelea kudumisha amani ya nchi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu visiwani humo. https://youtu.be/lixj9MuX_ak

Simu.tv: Shirika la maendeleo la kimataifa UNDP labainisha malengo yake hapa nchini ikiwemo kusaidia taasisi mbalimbali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi. https://youtu.be/tX_jZ1iw4Wg

Simu.tv: Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo afanya ziara wilayani Mwanga na kutilia shaka gharama zilizotumika kujenga mradi wa umwagiliaji ikiwemo gharama zilizotumika kununulia mashine baada ya kubaini mapungufu kadhaa. https://youtu.be/HifnPmkby5U

Simu.tv: Naibu waziri wa maji na umwagiliaji ambana mkandarasi aliyeshindwa kukamilisha mradi alioingia mkataba mkoani Kigoma kufuatia taarifa za kufilisika kwake. https://youtu.be/TVz8ENGvuYk

Simu.tv: Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa abainisha juhudi za serikali katika ujenzi wa darasa la mto Kilombero ili kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo. https://youtu.be/z72KlVDUvL8


Simu.tv: Mtu mmoja afariki dunia na lori moja kuteketea kwa moto baada ya moto kulipuka katika kituo cha mafuta wakati wa upakiaji wa mafuta kiutoni hapo mkoani Rukwa. https://youtu.be/Hirww7eMAhw

Simu.tv: Serikali yaombwa kulipa malimbikizo na madeni ya walimu yaliyochueleweshwa kwa muda mrefu pamoja na kuboresha makazi yao ili waweze kufundisha kwa ufanisi zaidi.

Simu.tv: Taasisi ya Mkapa Foundation chini ya ufadhili wa mfuko wa dunia wa kupambana na Ukimwi yakabidhi nyumba 60  zilizojengwa mkoani Lindi ili kupunguza uhaba wa nyumba kwa watumishi wa afya.https://youtu.be/zC7NkmJSEw0

Simu.tv: Zaidi ya shilingi milioni 600 zilizotolewa na Rais wa awamu ya 4 kwa ajili ununuzi wa gari la wagonjwa wilayani Bunda zaelezwa kutumika kinyume na malengo huku TAKUKURU ikitakiwa kufanya uchunguzi wa kina na kuwafikisha wahusika mahakamani. https://youtu.be/SyzpcyfKrcA

Simu.tv: Baada ya Mtibwa Sugar kuibuka na ushindi nyumbani hapo jana, Leo hii klabu Simba inashuka  dimbani kujihakikishia mbio za ubingwa. https://youtu.be/3XKlMLcv0E4

Simu.tv: Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF laazimia kuanzisha ligi kuu ya soka ya wanawake na vijana chini ya miaka 20 ifikapo mwezi wa 8. https://youtu.be/ApK58UK197s

No comments: