Monday, March 7, 2016

HABARI KUTOKA TELEVISHENI


Simu.tv: Rais Magufuli amteua balozi John Kijazi kuwa katibu mkuu kiongozi kujaza nafasi ya balozi Sefue atakaye pangiwa kazi nyingine. https://youtu.be/ytP8aAXVDs0  

Simu.tv: Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu aeleza kwamba jeshi la polisi linaangalia jinsi likavyo imarisha nguvu katika kulinda miundombinu ya gesi ikiwemo visima na mabomba ya kusarifirishia nishati hiyo ili kuhakikisha nishati hiyo inainufaisha jamii na taifa kwa ujumla.https://youtu.be/ooKvYZE9rpY  

Simu.tv: Wizara ya Ujenzi yasema inakusudia kutuma timu ya wataalam kwa ajili ya kukagua na kufanya tathimini na kukagua gharama halisi zilizotumika katika ujenzi wa Gati ya bandari ya Pangani. https://youtu.be/DH00OZhRUzM  

Simu.tv: Wafanyabiashara wadogo mkoani Mwanza waziomba benki na taasisi za fedha kuwakopesha mitaji mikubwa na vitendea kazi vya kibiashara ili waweze kuondoka katika kada ya biashara ndogo. https://youtu.be/3myNBMmdGSQ  

Simu.tv: Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli awaomba watanzania na mashirika mbalimbali nchini kutambua kwamba kila mmoja ana wajibu wa kuwasaidia wazee na wale wenye mahitaji.https://youtu.be/xsZSZqbHslM  

Simu.tv: Mbunge wa Meatu amuomba waziri mkuu kuchukua hatua stahiki dhidi ya mwekezaji anayejihusisha shughuli za uwindaji wilayani humo kwa kuwadhalilisha wananchi.https://youtu.be/lRBil29JiUg  

Simu.tv: Rais wa Vietnam anatarajiwa kuwasili nchini siku ya jumanne kwa ziara ya kiserikali ya siku 3 yenye lengo la kuhimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na Vietnam.https://youtu.be/iL92Q-yLt7s  

Simu.tv: Rais Dkt. John Magufuli atangaza kumteua Balozi Mhandisi John Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ; https://youtu.be/jgHPhwke0ak   

Simu.tv: Wadau wa sekta ya afya jijini Arusha wametoa msaada wa mashine mbili kwa ajili ya watoto Njiti katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru mkoani humo; https://youtu.be/S3-C_fOPzqs  

Simu.tv: Watumishi kumi na moja wa hospitali ya rufaa ya Sekou-Toure  wilayani Nyamagana wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa sababu ya kifo cha mama na watoto wake wawili mapacha; https://youtu.be/uNzYDNtthLQ  

Simu.tv: Serikali yafuta leseni ya uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo la Mgogo Sekenke mkoani Singida kutoka na mgogoro uliopo baina ya mwekezaji na wachimbaji wadogo;https://youtu.be/LkbUsuQ6YU8  

Simu.tv: Serikali yawataka wananchi kuondoa hofu juu ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga Tanzania; https://youtu.be/bAexY5IJVZI  

Simu.tv: Jeshi la polisi nchini limesema litaongeza nguvu kazi ya ulinzi wa visima na mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam; https://youtu.be/hsSfaiaLfSg  

Simu.tv: Waziri mkuu Kassim Majaliwa asitisha ziara yake mkoani Simiyu  kufuatia kifo cha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Maswa; https://youtu.be/6KXwUs26MYo  

Simu.tv: Serikali mkoani Tabora yaendesha harambee kwa ajili ya kuchangia madawati katika shule zinazokabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati; https://youtu.be/TuEPBve21jg  

Simu.tv: Inaelezwa kuwa Rais wa Vietnam anatarijia kuzuru Tanzania mnamo tarehe 8 mwezi huu kwa  ziara ya siku tatu; https://youtu.be/E0EPLrvZPTw   

Simu.tv: Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi  madereva  nchini, Shabani Mdemu awatoa wasiwasi walimu kuhusu suala la kusafiri bure wanapokuwa wanaelekea kazini au kutoka kazini;https://youtu.be/_F3OGwaxJ9Q  

Simu.tv: Timu ya Simba yaitandika timu ya Mbeya City kwa jumla ya goli 2 kwa 0 katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliofanyika hii leo jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/uAprUpnti0c  

Simu.tv: Benchi la ufundi la timu ya taifa ya soka ya wanawake Twiga Stars limesema Twiga Stars bado ina nafasi kubwa ya kusonga mbele  katika michuano ya awali ya kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika kwa wanawake; https://youtu.be/WQdMviTH0GM

No comments: