Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza uongozi wa Hospitali y teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi kuanza kutumia jokofu moja lenye uwezo wa kuchukua miili nane (8) katika chumba cha kuhifadhi maiti (Mochwari) ya Hospitali hiyo baada ya kuridhishwa na hatua iliyofikiwa baada ya kutembelea kwa mara ya pili kuikagua, tokea alipoipa masaa 72 ifungwe na ifanyiwe matengenezo.
Dk. Kigwangalla alifika hospitaalini hapo majira ya saa nane mchana na kisha kwenda moja kwa moja kwenye jingo hilo la Mochwari na kukuta mafundi wakiendelea na matengenezo kwa upande wa majokofu ambayo yalikuwa hayafanyi kazi na kusababisha matatizo hata Naibu Waziri kuagizwa kufungwa ma siku tatu ili uongozi huo ufanyie matengenezo.
“Nilitoa masaa 72, muwe mumefanyia kazi tatizo hili. Na leo hii nimerudi tena kukagua kuona utekelezaji wa agizo langu kama mumelifanyia kazi. Hivyo kwa kuwa tayari ili jokofu moja limeanza kutengamaa nalifungulia lianze kazi mara moja na la pili lianze kazi pia litakapokamilika mutujulishe haraka sana” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Tumbi.
Ziara hiyo katika kukagua utekelezaji wa Mochwari hiyo ya Tumbi, ameifanya jana Machi 13.2016 akiambatana na maafisa wa Wizara yake hiyo ambapo pia alipata kutembelea Hospitali nyingine ya Jijini Dar es Salaam ya Sanitas ambayo imefungiwa kutoa huduma kwa upande wa chumba cha Upasuaji kutokana na kutokidhi vigezo.
Hata hivyo kwa upande wa Hospitali Dk. Kigwangalla alieleza bayana kuwa, alipata taarifa juu ya uongozi wa Hospitali hiyo kuendelea na huduma za upasuaji lakini hakukuta hali hiyo na kuendelea kusisitiza huduma hiyo isifunguliwe mpaka hapo watakapokamilisha vigezo vya Wizara juu ya Chumba chaa upasuaji kinavyotakiwa kiwe.
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog.
Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akiangalia namna utengenezaji huo unavyoendelea kwa upande wa nje wa majokofu hayo.
Mtaalam wa upande wa Mochwari hiyo ya Tumbi akitafakari jambo wakati wa ujio huo wa Naibu Waziri Dk. kigwangalla.
No comments:
Post a Comment