Thursday, March 3, 2016

CCM MKOA WA ARUSHA YAMCHAGUA LEKULE KUWA MWENYEKITI ,HUKU SHABANI MDOE AKIIBUKA KATIBU MWENEZI

SAM_7665
Mwenyekiti mpya wa ccm mkoa wa Arusha   Maiko Lekule aliyepata kura 515akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti hicho hivi karibuni jijini Arusha(Habari  Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_7696
Katibu mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Arusha Shabani Mdoe aliyeshinda na fasi hiyo kwa kupata kura 36 ambaye kwa taaluma ni mwandishi wa habari akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa mkutano huo mara baadaa  ya kutangazwa rasmi kushinda nafasi hiyo
SAM_7636
Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm taifa Stephen Wassiraakitangaza rasmi nafasi ya mwenyekiti wa mkoa ambapo pia aliwataka wanaccm kuhakikisha wanashirikiana
SAM_7656
Mjumbe wa NEC taifa toka wilaya ya Monduli Namelock Sokoine akizungumza katika mkutano huo mara baada ya uchaguzi kuisha ambapo aliwataka wanaccm kuchapa kazi na kuhakikisha wanawashuhulikia mamluki waliopo ndani ya chama hicho
SAM_7676
Mjumbe wa NEC taifa toka wilaya ya Monduli Namelock Sokoineakiteta jambo na Mbunge viti maalum Catherine Magige katika mkutano huo
SAM_7680
Emanuel Makongoro ambaye alikuwa akiwania nafasi wa uwenyekiti wa mkoa akifurahia jambo na katibu wa wazazi mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau 
SAM_7689
Semi Kiondo ambaye alikuwa akiwania nafasi ya ukatibu mwenezi akizungumza mara baada ya uchaguzi kuisha ambapo alihaidi kutoa ushirikiano wake kwa chama cha mapinduzi huku akishirikiana na viongozi waliochaguliwa
SAM_7684
viongozi wa chama cha mapinduzi wakiwa katika pozi la picha
SAM_7630

Wajumbe wa mkutano
 CHAMA cha Mapinduzi ( CCM)mkoa wa arusha kimefanya uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa  na kufanikiwa kumchagua  Maiko Lekule aliyepata kura 515 dhidi ya mgombea mwenza Emanuel Makongoro aliyepata kura 338,huku katibu mwenezi wa chama hicho akichaguliwa kuwa ni Shabani Mdoe aliyeshinda na fasi hiyo kwa kupata kura 36.

Aidha katika uchaguzi huo wa mwenyekiti  wajumbe  halisi waliopaswa kuhudhuria  ni 960 ambapo waliohudhuria ni 903 huku wajumbe halisi waliopiga kura wakiwa ni 861.

Akitangaza matokeo hayo jana msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm taifa Stephen Wassira alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa huru na amani na hivyo ana imani kuwa uongozi huo utakiletea mabadiliko makubwa chama cha mapindizi katika mkoa huo.

Alisema kuwa katika mkoa wa arusha matatizo ya umoja  na tofauti yapo na kwamba atakayemaliza mzizi huo ni mwenyekiti aliyepatikana kwa kuhakikisha kuwa anawaunganisha wana ccm ili wawe kitu kimoja.

“hapa arusha yapo matatizo sana naomba tu nitumie fursa hii kumtaka mwenyekiti aliyeshinda kuhakikisha kuwa anakijenga chama na ndie atakayeifanya arusha iungwe mkono na watu wote hatutaki kusikia tena kuwepo kwa makundi ya kuvunja chama muda wa uongozi wa mwaka mmoja ni mkubwa sana katika kukirejesha chama sehemu yake”alisema Wassira.

Alileleza kuwa kwa arusha hawataki  kusikia ccm  inayoendeshwa kwa fedha ya mtu binafsi wala kampuni bali wanaitka ccm yao irudishe kwa wananchi na jamii iweze kunufaika na rasilimali zake sio kwa ajili ya watu binafs ambao  ndio wamekuwa wakikisaliti chama.

Kwa upande wake mwenyekiti aliyechaguliwa Maiko Lekule  akitoa neno la shukrani  alisema kuwa anawashukuru wajumbe hao kwa kumchagua na kwamba nafasi aliyopewa hataweza mwenyewe kuimaraisha chama hicho ambacho kipo mahututi hivyo anaomba ushirikiano uwepo.

Lekule alisema kuwa chama hicho kinahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa sana hivo kamati za siasa ,wenyeviti na kamati inabidi waungane kwa pamoja kukijenga chama hicho kwa upya ili kirudi katia hali yake.

“mimi nahidi tu ntakiimarisha chama hiki kwa kushirikiana na wenzangu ila niwaombe tu mamluki wote walioko kwenye hiki chama ambao ndio wasaliti wakuu waondoke mapema wenyewe na kama hawataondoka tutawaondoa sisi”alisema Lekule.


Nae katibu mwenezi Shabani mdoe ambaye ni mwandishi mwandamizi wa gazeti la Uhuru  aliwashukuru wajumbe hao kwa kumuamini kwa kumchagua na kuahidi kuwa atatumia taaluma yake ya uhabari kuimarisha chama hicho kwani waandishi wana nguvu kubwa ya kujenga palipobomoka.

No comments: