Kampuni ya wino na vifaa vingine vinavyotumika katika uchapaji ya Cartridge World yenye makao yake makuu Hong Kong nchini China imezindua duka la vifaa hivyo jijini Dar es Salaam lengo likiwa kusaidia kupunguza gharama za uchapaji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Cartridge World, Rajesh Pandya alisema kuanzishwa kwa duka hilo nchini kutasaidia kupunguza gharama za uchapaji kwani wino na vifaa vingine vya uchapaji vya kampuni hiyo sasa vitapatikana kwa bei nafuu.
Alibainisha kuwa kampuni hiyo itakuwa pia inatengeneza vifaa hivyo nchini vikiwa katika ubora unaoitambulisha kampun I hiyo ulimwenguni ambako ina matawi katika nchi 50 ulimwenguni na maduka zaidi ya 700 Marekani na 130 nchini Uingereza.
Alisema unafuu wa bei utawezesha kushuka pia kwa gharama za uchapaji na hivyo kuwapa nafuu wahitaji wa huduma za uchapaji na pia katika kuliepusha Taifa na uharibifu wa mazingira, kampuni hiyo itakusanya vifaa vilivyotumika hususan vya kuhifadhia wino na kuviteketeza.
Alisema duka litrakuwa na matawi katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza kwa kuanzia na wigo zaidi utapanuliwa ili kutosheleza mahitakji ya huduma za Catrtridge nchini.
“Kifaa cha kuhifadhi wino katia mashine ya uchapaji kikitupwa ardhini kinaweza kuchukua hata miaka 400 hadi kuharibika hivyo kampuni yetu ulimwenguni kote inakusanya vifaa hivyo vilivyotumika na kuziunda upya kabla ya kuviingiza tena sokoni lengo likiwa kuepusha uharibifu wa mazingira” alisema.
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Mandeleo ya biashara Kimataifa, Harry Stoubos alisema kufunguliwa kwa duka hilo nchini ni njia ya kuingia katika soko la Afrika Mashariki na Tanzania ndio nchi pekee ukanda wa Afrika Mashariki ambako duka linafunguliwa.
“Tanzania ndio nchi ya kwanza Afrika Mashariki na tunatarajia kupanua wigo zaidi katika ukandaa huu ili tuwe na martawi katia nchi zote za Afrika Mashariki” alisema na kuongeza kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ndio ambayo imewavutia kuwekeza nchini.
Ofisa Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni ya Cartridge,Harry Stoubos (kushoto), akimkabidhi kabrasha Mkurugenzi Mtendaji wa Catridge World-Africa Mashariki, Rajesh Pandya ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa duka la vifaa kuhifadhia wino katika mashine za uchapaji vya kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Cartridge World kwa Africa Mashariki, Rajesh Pandya na Ofisa Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni hiyo,Harry Stoubos wakionyesha kwa waandishi wa habari vifaa vya kuhifadhia wino katika mashine za uchapaji wakati wa uzinduzi wa duka hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara –Afrika Mashariki wa Kampuni ya Cartridge World, Ashish Nagewadia (kushoto), akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa duka hilo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji kampuni hiyo, Africa Mashariki, Rajesh Pandya na Ofisa Mkuu Kimataifa, Harry Stoubos.
Mkurugenzi Mtendaji wa Cartridge World kwa Africa Mashariki, Rajesh Pandya (kulia) na Ofisa Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni hiyo, Harry Stoubos wakikata keki kuashiria uzinduzi wa duka hilo leo.
Ofisa Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni hiyo, Harry Stoubos (kushoto) akijadiliana jambo na Komal Nagewadia ambaye ni msaidizi mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, wakati wa uzinduzi a duka hilo.
No comments:
Post a Comment