Friday, March 4, 2016

Balozi wa Norway atembelea Mkoa wa Iringa

​Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad, amefanya ziara ya siku 2 Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Kilolo na Wilaya ya Iringa na kufanya shughuli ya kuzindua shule ya watoto ya awali inayofundisha mwa mfumo wa Montesori.

Shule hiyo iliyopo Ilula, katika wilaya ya Kilolo inafadhiriwa na wanachi wa Norway kupitia kwa mdau wa Maendeleo Norway na familia yake Bw. Osmund pamoja na wananchi wengine ambao wameunda NGO iitwayo Ilula Orphanage Program (IOP) chini ya Mwenyekiti wake raia wa Marekeni Bibi Berit Skaare.

Akimkaribisha Balozi kuzindua Shule hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, alisifu na kushukuru wananchi wa Norway kwa kazi kubwa wanayofanya Tanzania hasa katika elimu, Pia alipongeza juhudi za wananchi wa Norway wanavyo jali watanzania.

Kasesela aliagiza Halmashauri kutunza kituo hicho na kuhakikisha kinaendelea kuwa bora na kufundisha watoto wetu, Pia aliagiza Halmashauri iangalie uwezekano wa kutengeneza barabara ya kufika kituoni hapo kwani kwa sasa hairidhishi. 

Nae Balozi wa Norway nchini, Hanne Marie, alishukuru serikali ya Tanzania na kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kasi anayokwenda nayo kukomboa elimu. Pia alishukuru Mkoa wa Iringa kwa kutoa ardhi ili ijengwe shule hiyo ya kisasa. Balozi aliaahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika nyanja ya elimu hasa elimu ya ufundi stadi.

Balozi aliendelea na ziara yake kukagua miradi ya REA ambayo baadhi inafadhiliwa na serikali ya Norway. Atatembelea mradi wa Mgama ulioko kata ya Lumuli Iringa.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad akiwa na Mwenyeji wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Shuleni hapo tayari kwa uzinduzi rasmi.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, wakiangalia umahiri wa Mtoto Martha katika kutaja mikoa ya Tanzania aliyokuwa akiitaja kwa kuonyesha ramani.
Mtoto Anderson akifuahia jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa shule hiyo.
watoto wa Sallirud Montesori Ilula wakiimba ​

No comments: