Sehemu ya Barabara ya Morocco kwenda Mwenge ikiwa katika hatua ya kutolewa tabaka ya udongo wa chini na kuwekwa tabaka ya udongo mpya kama inavyooenekana katika picha leo jijini Dar es Salaam .
Mafundi kutoka kampuni ya Ujenzi ya ESTIM wakiwa kazini katika hatua ya kutoa udongo wa chini kwa ajili ya kuweka udongo mpya ,ambapo ujnzi huo unatarajiwa kumalika mapema Mei mwaka huu.
Mafundi wakijengea bomba la maji eneo la Makumbusho kwa kuliwekea zege na nondo ili kulihakikishia usalama wake wakati wa ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco inayotarajiwa kukamilika mapema mwezi Mei mwaka huu.
Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Bi.Aisha Malima akipata maelezo kutoka kwa Fundi Mchundo (Civil Technician) wa Kampuni ya Ujenzi ya ESTIM ,Bw. Kano Warema kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco leo jijini Dar es Salaam.
Kipande cha Barabara ya Mwenge-Morocco kilicho kamilika kwa kiwango cha lami katika eneo la Mwenge-Bamaga kinavyoonekana katika picha . (Picha na Lorietha Laurence –Maelezo).
No comments:
Post a Comment