Monday, February 1, 2016

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YAWAKOMBOA WANAWAKE WA ZANZIBAR KIUCHUMI

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser .
Taaasisi ya Manjano Foundation inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Wanawake wa mjini Zanzibar. Taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kumkomboa mwanamke aweze kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.Katika mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Hotel ya Mtoni Marine Zanzibar wanawake  hao watapatiwa elimu namna ya kuanzisha na kuendesha biashara. Pia watajifunza  namna ya kujiwekea akiba na kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao. 
Mwisho wa mafunzo haya washiriki wote watakopeshwa mitaji kwa ajili ya kuanzisha na  kuendesha biashara zao. Katika hatua nyingine washiriki wa mafunzo hayo waliojitokeza kwa wingi wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwakomboa na mafunzo ya kiuchumi na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Washiri wa mafunzo hayo..
Mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza  washiriki watapewa mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha biashara, pia kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao kwenye jamii wakiwa kama wanawake na kuondoa woga wa kujihusisha na kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika biashara zao ambapo Mkufunzi wa masomo hayo ya maswala ya Biashara ni Mama Salma Salim Omar wa Zanzibar Chamber of Commarce.
  
Baadaye mtaalamu wa maswala ya urembo na matumizi ya sahihi ya vipodozi Mama Shekha Nasser atatoa ujuzi wa matumizi ya vipodozi pendwa vya LuvTouch Manjano, mfano kupamba maharusi na utunzaji wa ngozi.
Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Zanzibar 
waliojitokeza kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali.

No comments: