Monday, February 22, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI LEO

Waziri mkuu mhe.Kassim Majaliwa aiagiza serikali ya mkoa wa Iringa kupitia kamati ya maafa kuhakikisha wananchi waliohamishwa kwenye maeneo yaliyoathirika na mafuriko hawarudi tena kwenye maeneo hayo.https://youtu.be/jJbqU6FwnAQ
  
Waziri Angela Kairuki atumbua majipu baada ya kumsimamisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma nchini pamoja na watumishi 2. https://youtu.be/1lJ3_LtjyT4  

Katika hali ya kusikitisha mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 4 aishiye mkoani Mpanda achomwa moto na baba yake mzazi kwa madai ya kuiba mboga aina ya chainizi.https://youtu.be/UZBzT5HU0is  

Kampuni ya Vodacom yaendela kupanua huduma zake nchini na kutoa nafasi za ajira baada ya kufungua duka lake jipya mkoani Arusha. https://youtu.be/IhXCiEx-Jws

Serikali yaanza kuchukua hatua madhubuti katika kutatua mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Mvomero baada ya pande hizo kukubaliana kuweka mpaka utakao tenganisha maeneo ya wakulima na wafugaji. https://youtu.be/f7eSFHlwOKU  

Wafanyabiashara katika mji wa mbinga mkoani Ruvuma wafanya usafi wa mji huo kwa kuzoa taka zote zilizozagaa mitaani hatua iliyopongezwa na wakazi wa mji huo. https://youtu.be/k17-d6tC2-I  

Huduma ya afya ya mama na mtoto katika maeneo ya vijijini yaelezwa kuwa bado ni changamoto kubwa kufuatia mazingira magumu ya kazi. https://youtu.be/bIuP_0v8YLA  

Serikali yaombwa kuingilia kati ili kunusuru kilimo cha pamba kwa kuwasogezea wakulima pembejeo baada ya hapo hawali kuuziwa mbegu zilizooza. https://youtu.be/v-gMDVUul1w  

Serikali yakusanya kiasi cha shilingi Tririoni moja kwa mwezi Februari ambazo tayari imezipeleka katika shughuli mbalimbali ya maendeleo; https://youtu.be/mfV3aHyg2sk  

Halmashauri ya manispaa ya Temeke yaanza ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi ya Majimatituhttps://youtu.be/6Qh_1yD42Tk  

Inaelezwa kuwa takribani shule za msingi arobaini na saba zilizojengwa na wananchi walayani Kaliua  mkoani Tabora hazijasajiliwa; https://youtu.be/1QPlUknn9Cg  

Waziri mkuu Kassim Majaliwa awatembelea wananchi waliokumbwa na mafuriko katika tarafa ya Pwaga wilayani Iringa;https://youtu.be/q73xgi9r_RA  

Serikali ya Canada yaikabidhi SIDO msaada wa kiasi cha shilingi bilioni 23 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vinne vya mafunzo ya  ujasiriamali; https://youtu.be/VaAhAiiW2Q0  

Serikali yalitaka baraza la uwezeshaji kiuchumi wananchi kuhakikisha linafikia malengo yake ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana; https://youtu.be/SSZtpf82hKI  

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alex Sanchez amesema hajutii uamuzi wake wa kuima klabu ya Barcelona na kujiunga na Arsenal;https://youtu.be/03_cKhTRvyU  

Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC yaanza kutoa mafunzo kwa watendaji watakaosimamia uchaguzi wa marejeo utakaofanyika mwezi wa tatu mwaka huu; https://youtu.be/5wLl7yuYps8  

Rais Dkt Ali Mohammed Shein awataka vijana wa Chama Cha Mapinduzi visiwani Zanzibar kuendelea kulinda mapinduzi na kudumisha muungano; https://youtu.be/NgwcB6kYb40

No comments: