Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee tayari kwa kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo ambapo mkutano huo pia ulihudhuriwa na Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amehudhuria katika mkutano huo ambapo alionekana mtu mwenye kufurahia hotuba hiyo.
Mwanzoni Askofu Gwajima alipofika ukumbini hapo alikuta ratiba inaendelea hivyo ilibidi akae viti vya nyuma lakini Shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim alimpigia simu na kumwomba aende mbele akakae pamoja na viongozi wenzake wa dini.
(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo wakati alipoongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es salaam mzee Hemed Mkali kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Mh. Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es salaam wa zamani Mzee Idd Simba, Kulia ni mfanyabiashara Abdullah Mohamed.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa na Mke wa Rais Mama Janet Magufuli wakiwa meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam.
Baadhi ya mawaziri wa wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya tano wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo na ya Kiislamu wanaounda kamati ya Amani wakiwa katika mkutano huo
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hakubaki nyuma na yeye amehudhuria katika mkutano huo na hapa akionekana mwenye furaha na bashasha kama alivyonaswa na kamera yetu.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amekaa pamoja na viongozi wenzake wa dini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam wakati Rais Dk. John Pombe Magufuli alipozungumza na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
Baadhi ya wazee wa Dar es salaam wakitambulishwa katika mkutano huo.
Baadhi ya mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo kutoka kulia ni Mh. Profesa Sospeter Muhongo, Dk. Abdallah Posi, Nape Nnauye, Januari Makamba na Ummy Mwalimu.
Baadhi ya wazee wakifuatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano huo.
Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimia wazee katika mkutano huo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wazee katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es alaam Mzee Hemed Mkali akihutubia katika mkutano huo na kumkaribisha Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kuwahutubia wazee hao.
Wazee hawa wakionekana kuhamasika na hotuba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
No comments:
Post a Comment