Monday, February 15, 2016

POLEPOLE ASEMA DC KASESELA NI HAZINA YA TAIFA, UTUMBUAJI WA MAJIPU WA RAIS DR MAGUFULI WAPO WANAOUMIA ILA WAWE WAPOLE

Bw Polepole akimpongeza mkuu  wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela wakati wa kongamano la shirikisho la vyuo vya elimu ya  juu la  wana CCM mkoa wa Iringa jana
.Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw  Richard Kasesela akiwa amembeba mmoja kati ya watoto wakazi wa  kijiji  cha Mboliboli tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa ambao wamekumbwa na mafuriko ambayo maji yake yana vimelea  vya ugonjwa wa kipindupindu  kwa  zaidi ya  siku nne sasa baadhi  yao bado wanaishi juu ya vichuguu
Mkuu  wa  wilaya ya Iringa akizungunza na wananchi  waliookolewa katika mafuriko Pawaga
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw Richard Kasesela akizungumza na  wanafuzi  wa vyuo vikuu mkoa  wa Iringa  wakati wa kongamano la jana kushoto ni Bw Polepole na kulia na kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Bw  salim Asas  na katibu  wa shirikisho hilo Bi mariam Fundi 

Na MatukiodaimaBlog
ALIYEKUWA mjumbe  wa  tume ya mabadiliko  ya katiba  BW Humphrey Pole pole amempongeza mkuu  wa  wilaya ya Iringa  Bw Richard Kasesela kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kujitoa kunusuru uhai  wa wananchi  wa kata ya Mboliboli tarafa ya Pawaga  ambao wamekubwa na mafuriko yenye vimelea vya  ugonjwa  wa kipindupindu  kuwa mkuu  huyo wa  wilaya  ni hazina kubwa ya  Taifa  na  kumwomba Rais Dr John Magufuli kumkumbuka katika ufalme wake.
Huku akidai kuwa kazi  inayoendelea kufanywa na rais Dr Magufuli ya  kutumbua majipu wapo ambao wanaumizwa zaidi kutokana na kupoteza imani ya kuendelea kuishi maisha ya kula bata kila  uchwao.
Bw Polepole ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano la miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM na siku  100 za Rais Dr Magufuli lililoandaliwa na  shirikisho  la vyuo  vya  elimu ya  juu la chama cha Mapinduzi (CCM)  mkoani  Iringa lililofanyika  jana  mjini hapa alisema  kuwa amepata kushuhudia kupitia vyombo vya habari mbali mbali jinsi ambavyo mkuu  huyo wa wilaya ya  Iringa Bw Kasesela anavyojitolea  kuokoa maisha ya wananchi wake jambo ambalo kwa viongozi  wengine ni vigumu kufanya  hivyo.
Alisema kuwa kati ya wakuu  wa  wilaya ambao wamekuwa wakiitambua kazi yao kwa wananchi na wananchi wakiona bila tatizo kazi inayofanywa na kiongozi  wao ni pamoja na mkuu  huyo  wa wilaya ya Iringa ambae ushujaa na uzalendo  wake kwa  wananchi  wake ni mkubwa na mfano  wa  kuigwa na viongozi wengine katika kuwatumikia  wananchi.
" Tanzania  ya Rais Dr Magufuli itapiga hatua  kubwa  zaidi ya leo  tunapotathimini siku 100  za utawala  wake  iwapo watendaji  wote  watatambua wajibu  wao kwa  wananchi wao badala ya kutangulia maslahi yao kwa  taifa yao....nimependezwa  sana na moyo  wa  kujitolea kwa ajili ya wananchi ambao mkuu huyu wa wilaya kakangu Richard Kasesela anaonyesha ni mmoja kati ya wakuu  wa wilaya ambao wanafanya kazi kwa  moyo .....nimeona katika mitandao ya  kijamii mkuu  huyu wa  wilaya akiogelea katika maji kuokoa maisha ya wananchi  wake ambao wamekubwa na mafuriko tena maji yenye vimelea vya  kipindupindu ....ni nani angeweza kuhatarisha maisha yake  hivi zaidi ya kutuma waliopo chini yake kufanya kazi kwa niaba  yake" alihoji Bw polepole.
Huku akimtaka  mkuu   huyo  wa  wilaya  kuzidi  kutumika vema kwa ajili ya  wananchi  wake na  kuomba iwapo inawezekana Rais Dr Magufuli kwenye utumbuaji  wake  wa majipu kwa wakuu  wa  wilaya na mikoa kuangalia wakuu  wa wilaya wasio tambua wajibu  wao ambao wapo kwa ajili ya faida  yao na  kuwaacha ama  kuwapandisha vyeo  zaidi   wale ambao wamekuwa wakifanya  vizuri.
" Simpigii debe Kasesela  ila naongea ukweli ulio  wazi kwa  kila mmoja wenu hasa  watu  wa Iringa ambao mmekuwa  nae ....binafsi nimevutiwa na utendaji  wake mzuri nampongeza  sana".
Hata  hivyo Bw Polepole  alisema  kuwa kazi  inayofanywa na Rais Dr Magufuli ya kutumbua majipu ni kazi ya nzuri  kwa  watanzania  swapenda uzalendo ila wapo  wanaoumia kwa ndugu  zao ama wenyewe kutokuwa na uhakika  wa  kuendelea  kufanya anasa za matumizi ya pesa ama kupata mkate wa  kila  siku.
" Hii  ni kazi nzuri sana na inapaswa  kuendelea  kwa nguvu zote ...ila tuwe  wakweli hapa wengi  tunashangilia  kuona majipu ambayo si ndugu  yanatumbuliwa hivi inakuwaje kama zamu ya  kutumbua jipu ingekuhusu wewe ama mzazi  wako .....bila shaka ungeona  zoezi hili ni baya  zaidi lakini kwa  ajili ya  kuifanya Tanzania kuwa ya  wote lazima  tuwe wapole tuache kila jipu  litumbuliwe  kwa afya yako ".
Aidha  alisema utendaji mzuri  wa Dr Magufuli na  serikali yake ya CCM umepelekea wapinzani nchini  kukosa hoja ya kuzungumza na kuendelea  kuokoteza maneno ya  kuongea ili mradi  waonekane wameongea jambo lakini kimoyo  moyo  wanapongeza kazi nzuri ya serikali ya CCM chini ya rais Dr Magufuli.
Pia alipongeza imani  kubwa ya  wanachama wa chama  cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kutoka  vyuo vikuu vya  Iringa ambao wamehama  vyama  hivyo na  kujiunga na CCM baada ya kupendezwa  na utendaji mzuri  wa Rais Dr Magufuli katika  kutekeleza Ilani ya  CCM na  kuwataka wengine kuzidi kurudi CCM kwani wapende  wasipende kasi ya rais Dr Magufuli ni  kubwa tofauti na  walivyotegemea.
Kwa  upande  wake  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw kasesela pamoja na  kumpongeza Bw polepole kwa kuendelea kuelimisha  umma kupitia vyombo mbali mbali  vya habari  juu sera  nzuri  za CCM na  kutambua kazi anayoifanya yeye kama mkuu  wa wilaya ,bado  alitaka wasomi nchini  kutokubali kupandikizwa siasa chafu  za kulalamika na kutuhumu kila uchwao na badala  yake  wao kuwa msaada kwa umma.
Alisema  wapo baadhi ya  wana siasa  wanatumia wasomi kuhadaha  umma kwa faida  yao badala ya  kuelimisha  umma kwa  kueleza ukweli nini CCM imefanya kwa  miaka yake 39.
" wapo  baadhi ya wanasiasa wao kazi kwao ni kusema ovyo ovyo  serikali ya CCM na  wengine wapo hadi Iringa ambao  wao bila kutukana ama  kuisema vibaya  serikali ya CCM kwao  siku haijapita .... binafsi sitanyamaza kuona mwana siasa ama mtu  yeyote akimsema ovyoovyo  Rais wangu Dr John Pombe Magufuli kama akiongea mbele  yangu ngumi moja  mbili nitampa na akiongeza mbali ya mimi kama katika vyombo  vya habari nitamjibu haraka.....siwezi hata  siku moja  kuvumilia mtu msema ovyo heri hata  huu ukuu  wa wilaya  nipoteze kwa kuitetea serikali yangu  ya CCM"




No comments: