Sunday, February 14, 2016

Nyumba za Kaya zaidi ya 80 za kitongoji cha kitanewa, kijiji cha mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa zatakiwa kuhama

Nyumba za Kaya zaidi ya 80 za kitongoji cha kitanewa, kijiji cha Mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa zipo hatarini kuathiriwa na mafuriko endapo hazitahama eneo hilo ambalo ndipo mkondo wa maji ya Mto mapogoro umechekupuka.
Kufuatia hali hiyo serikali Wilayani Iringa imewataka wananchi hao kuhama eneo hilo na kuhamia kwenye eneo lililotengwa kijiji cha Mapogoro hadi mvua zitakaposimama na kujenga makazi ya kudumu huko kijijini.
Taarifa zaidi na Irene Mwakalinga kutoka Iringa Hapa ni kazi ya kurejesha mkondo wa maji kwenye njia yake ya asili ikiendelea kwa kuchimba mchanga na kupanua kingo ya bonde ambalo mto umehamia na kuziba maji yasiendelea kwenda kwenye makazi ya watu.
Aidha Kinachoonekana hapa ni moja ya shamba la mahindi na karanga ambalo limegeuka mto na kumegwa ardhi yake na kasi ya maji ambayo inaendelea kula ardhi hiyo.
Afisa Tarafa wa Idodi Yakub Kiwanga amesema  kuwa mkondo wa maji ya Mto huo umehama kutoka eneo la mtitiririko wake awali na kukatisha kwenye maeneo ya makazi ya watu ikiwa ni miaka zaidi ya 40 tangu mto huo ulipohama tena.


Kijiji cha Itunundu ndio kambi kubwa ya uokoaji
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika wakati wa zoezi la  uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika wakati wa zoezi la  uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akikagua athari katika kijiji cha Mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akiendelea kukagua athari katika kijiji cha Mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa 

No comments: