Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akiongea na menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara
ya kuzitambua taasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akiongea wakati wa kikao na wafanyakazi wa Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam,
wakati wa ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake kushoto
ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TBA Arch.Elius Mwakalinga.
Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (hayupo
katika picha) leo jijini Dar es Salaam, katika ziara ya kuzitambua tasisi
zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Mhandisi. Manase Ole Kujan katika ziara yake ya kuzitambua
tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu
yanayotekelezwa na Taasisi hizo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
(Kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa
la Ujenzi (NCC) Mhandisi.Julius Mamilo(kulia) wakati ziara yake ya
kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu
yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani(Hayupo
katika picha) Mamilo katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya
wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo
jinini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, amezitaka
taasisi zilizo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uadilifu, bidii na kwa uharaka ili
kuendana na kasi ya madiliko ya Serikali ya awamu ya Tano.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara katika taasisi zilizo chini
ya Wizara yake ikiwemo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa lengo la kupata mafunzo
ya kiutendaji katika taasisi hizo.
Aidha amezitaka taasisi hizo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vya
mapato walivyonavyo na kamwe kutotegemea ruzuku kutoka Serikalini.
“Nataka ifikapo mwaka wa fedha ujao makusanyo ya mapato yawe yameongezeka zaidi
kuliko matumizi na kamwe msikae kusubiri ruzuku kutoka Serikalini, kikubwa ni kubuni
vyanzo vyengine vya mapato ili kuweza kujiendesha”, alisema Naibu Waziri.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa weledi na
bila woga kwani Serikali haitamuonea huruma yeyote anayekiuka kutekeleza wajibu
wake.
“Nawaomba mfanye kazi kwa morali kubwa ili kuweza kuisaidia jamii ambayo inahitaji
huduma muhimu kutoka Serikalini”, alifafanua Eng. Ngonyani.
Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA
Eng. Manase Ole kujan kutatua changamoto walizonazo ili kuleta mabadiliko chanya
katika taasisi hiyo.
“Una nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko hasa katika mfumo mzima wa ukatikatishaji
tiketi eneo la Magogoni ambalo limekuwa kero katika mfumo mzima wa ukusanyaji wa
mapato”, alisisitiza Naibu Waziri Ngonyani.
Sambamba na hilo Naibu Waziri amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo
Tanzania Arch. Elius Mwakalinga, kuandaa taarifa ambayo itaonyesha idadi ya nyumba
za Serikali wanazomiliki na ibainishe taarifa ya watumishi wenye stahili ya kupangishwa
kwenye nyumba hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole Kujan
amesema wakala huo umepanga kuboresha miundombinu hasa katika usafiri wa majini
na kuhakikisha inapunguza changamoto ya usafiri katika vivuko.
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Eng. Julius Mamilo
amebainisha changamoto walizonazo ikiwemo uhaba wa fedha hali inayosababisha
Baraza hilo kukwama katika kufanya kazi katika miradi yake ya maendeleo hususan
katika kufanya kazi za utafiti.
No comments:
Post a Comment