Thursday, February 4, 2016

MAANDALIZI YA CCM MIAKA 39 YASHIKA KASI MKOANI SINGIDA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari  ya Unyianga,kata ya Unyianga mkoani Singida.Shule hiyo mpya yenye madarasa manne ikiendelea kujengwa kwa nguvu za wanannchi.
Sehemu ya jengo la ujenzi wa maabara ukiendelea kwa nguvu za Wananchi
Badhi ya Wananchi waliokuwa wakishiriki ujenzi wa maabara hiyo,wakielekea kumsikiliza Katibu MKuu wa chama cha CCM Ndugu Kinana aliyefika katika shule hiyo ya sekondari ya Unyianga kushiriki ujenzi na kuwahimiza wananchi kushiriki kujenga maendeleo yao
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Unyianga mara baada ya kushiriki ujenzi wa shule hiyo,ambapo pia alimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Mhe.Joseph Mchina (kushoto) kufafanua baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kuwa kero kwa wananchi mpaka sasa na yamekuwa hayatimizwi kwa wakati.
Badhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa chama cha CCM Ndugu Kinana aliyefika katika shule hiyo ya sekondari ya Unyianga kushiriki ujenzi na kuwahimiza wananchi kushiriki kujenga maendeleo yao
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mhe.Mussa Ramadhan Sime akitoa ufafanuzi wa badhi ya mambo mbele ya Ndugu Kinana pamoja na Wananchi wa jimbo lake kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya wananchi waliofika kumpokea mapema leo asubuhi,alipokwenda kushiriki ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari  ya Unyianga,kata ya Unyianga mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa akiongozwa na mwenye shamba la Mtama Bwa.Elisha Abdallah sambamba na Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mussa Ramadhani alipokwenda kushiriki palizi la mkulima huyo wa mfano katika kata ya Mtamaa,mkoani Singida
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pichani kati akisukuma jembe la Plau linalokokotwa na N'gombe (kama aonekanavyo pichani) ikiwa sehemu ya kushiriki palizi katika shamba  hilo la Mtama lenye ukubwa wa Ekari moja na nusu  lililopo katika kata ya Mtama mkoani humo.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko mkoani Singida kwenye maandalizi ya sherehe za kuadhimishwa miaka 39 ya CCM,zinazotarajiwa kufanyika Februari 6 katika uwanja wa Namfua mkoani humo.
 Katibu Mku wa CCM Ndugu Kinana akiwa katika ukumbi wa ofisi za chama mkoa akisikiliza kero na mambo mbalimbali ya Wananchi ikiwemo kuyafanyia kazi,Ndugu Kinana amekutana na wajasiriamali (Mama Lishe,Boda boda,Wauza Mitumba na Wafanyabiashara nyingine ndogo ndogo. 
 Baadhi ya Wananchi wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea ndani ya ukumbi wa CCM Mkoa,uliowakutanisha wajasiria mali (Mama Lishe,Boda boda,Wauza Mitumba na Wafanyabiashara nyingine ndogo ndogo. 
 Wananchi wakifuatilia mkutano huo 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akitoa ufafanuzi kwa Wajasiria Mali hao mara baada ya kusikiliza kero na malalamiko mbalimbali ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo,ili kuendana kasi ya Rais Dkt Joseph Magufuli ya kuwahimiza wananchi kufanya kazi kwa kujituma kupitia kauli yake ya Hapa kazi Tu.

No comments: