Thursday, February 4, 2016

IBADA MAALUM YA KUMWOMBEA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,MH. DKT. MAGUFULI PAMOJA NA VIONGOZI WA TAIFA KWA UJUMLA – LUSAKA, ZAMBIA

Jumapili tarehe 31 Januari 2016 Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia ukishirikiana na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania uliandaa Ibada maalum iliyoendeshwa kwa ajili ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Uongozi mzima wa nchi na Taifa letu kwa ujumla.

Ibada hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya InterContinental Long Acres – LUSAKA.

Ibada hiyo Maalum ilifanyika kuanzia Saa saba mchana hadi kumi na mbili jioni na kuhudhuriwa na Watanzania wapatao mia tatu (300) wanaoishi Zambia wakifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na wafanyakazi na wafanyabiashara.

Viongozi wa dini na madhehebu ya Kikristo na Kiislamu walioshiriki kuendesha maombi katika Ibada Maalum hiyo ni: Brother Williamu Nyuki, Sheikh Suleiman Hussein, Mchungaji Noah Paulo na Mzee wa Kanisa Samuel Munata.
BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA , MH. GRACE MUJUMA AKISISTIZA JAMBO WAKATI WA HOTUBA YA UFUNGUZI WA IBADA MAALUM YA KUMWOMBEA RAIS WETU DKT JOHN POMBE MAGUFULI, VIONGOZI NA TAIFA KWA UJUMLA.
BALOZI MUJUMA AKIWASHUKURU WATANZANIA WALIOHUDHIRA IBADA MAALUM- LUSAKA, ZAMBIA.
BALOZI MUJUMA AKIWA NA VIONGOZI WA DINI IBADA MAALUM- BROTHER NYUKI NA SHEIKH HUSSEIN.
BAADHI YA VIONGOZI WA DINI IBADA MAALUM, PAULO, SHEIKH HUSSEIN NA MUNATA.
BALOZI MUJUMA AKIMPONGEZA MAKAMU MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WATANZANIA NCHINI ZAMBIA ROSE MULENGA BAADA YA IBADA MAALUM KUMWOMBEA RAIS NA TAIFA LETU.
BALOZI NA BAADHI YA WATANZANIA WALIOHUDHURIA IBADA MAALUM.
KWAYA IKIIMBA KWA HISIA.
WANA QASIDA IBADA MAALUM.

No comments: