Sunday, February 28, 2016

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI NCHINI


SIMU.TV: Nchi zinazounda jumuiya ya Afrika Mashariki zimeazimia kuanzisha vituo vya pamoja vya forodha ili kuondoa vikwazo katika biashara pamoja na kusafiri.https://youtu.be/kz_GFHmD3hk

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 39 kutoka Ethiopia pamoja na magari mawili waliyokuwa wakisafiria bila kuwa na vibali. https://youtu.be/0I12_FOANmI  

SIMU.TV: Waziri wa maliasili na utalii Prof.Maghembe asema serikali imejipanga vyema kupambana na uvunaji holela wa rasilimali za asili ikiwemo misitu na wanyama vitendo ambavyo vinaikosesha serikali mapato na uharibifu wa ikolojia.https://youtu.be/blPKbjYMGcE  

SIMU.TV: Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa afanya ziara kwenye bandari ya Mtwara na kubaini ubdhilifu huku akimuagiza mkuu wa bandari hiyo kuzuia uvujaji mkubwa wa fedha bandarini hapo. https://youtu.be/p6kEC-Etd9Q  

SIMU.TV: Uongozi wa mkoa wa Dar es salaam wamuaga rasmi aliyekuwa kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova aliyestaafu baada ya kuitumikia polisi kwa miaka 40. https://youtu.be/4y6-v7O-wdw  

SIMU.TV: Ugonjwa wa Kipindupindu waelezwa kupiga hodi wilayani Sumbawanga huku watu sita 6 wakilazwa na mmoja akiripotiwa kufariki dunia wakati akipaitiwa matibabu. https://youtu.be/MXNv-TQuqcA

SIMU.TV: Wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo mipaka ya vijiji vyao baada ya kukataa mipaka mipya waliyowekewa na wakala wa misitu Tanzania. https://youtu.be/w4doN_Nm2NU

SIMU.TV: Imeleezwa kuwa vifo vya akina mama na watoto havitapungua mkoani Geita endapo magari ya wagonjwa yanayomilikiwa na serikali mkoani humo yataendelea na kazi nyingine amabazo si zake. https://youtu.be/NQt06SuI5ns

SIMU.TV: Wafanyabiashara na wakulima nchini washauriwa kutumia simu za mkononi kujua bei za bidhaa na mazao na kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya maendeleo ya biashara zao. https://youtu.be/NmCX99DhS7c

SIMU.TV: Shirika lisilo la kiserikali la JHPIEGO lakabidhi jengo jipya la wazazi katika hospitali ya rufaa mkoani Mara ikiwa ni jitihada za kupunguza vifo vya mama na mtoto. https://youtu.be/hG2vnRVWdeM

No comments: