Mkurugenzi wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya Idarous Khamsin (katikati) akimtambulisha rasmi mwanadada, Wema Sepetu (kushoto) ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. (Kulia) ni Martin Kadinda ambaye naye miongoni mwa watendaji wanaoratibu jukwaa hilo la Lady in Red. katika usiku wa Lady In Red fashion show 2016, litakalofanyika 31 Januari ndani ya ukumbi wa Danken House wa Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Nyota wa filamu za Bongo, ambaye pia aliwai kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Wema Issac Sepetu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye onesho na jukwaa maalum la mitindo la kila mwaka la “Lady In Red 2016” litakalofanyika 31 Januari katika ukumbi wa Danken House uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya Idarous Khamsin amebainisha hilo alipokutana na badhi ya wabunifu wa mavazi na wanamitindo watakaopamba jukwaa hilo hiyo 31 Januari, ambapo amewataka kujipanga ilikuchangamkia fursa ya kupata kuinua tasnia ya mitindo nchini.
“Lady In Red fashion show 2016 ni ya kipekee na jukwaa hili ni fursa kwa kuinua wabunifu wa mavazi chipukizi kupata kuonekana zaidi na hata kukuza majina na ubunifu wao kujulikana ndani na nje” amefafanua Mama wa Mitindo, Asya Idarous.
Aidha, ameeleza kuwa, ilikutoa msisimko zaidi kwa jukwaa hilo. Mwanadada Wema Sepetu ndiye atakaye bariki siku hiyo ikiwemo utoaji wa vyeti kwa washiriki ilikuweka kumbukumbu.
Asya Idarous ameongeza kuwa, hadi sasa jukwaa hilo la Lady in red linafikia umri wa miaka 12 litaendelea kuwa juu zaidi na kuwa shule kwa tasnia ya mitindo ambapo kwa sasa pia linafanyika na nje ya Tanzania ikiwemo nchini Uingereza.
Hata hivyo wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza kuliunga mkono ikiwemo kudhamini onesho hilo.
Mkutano huo wa utambulisho wa jukwaa la Lady Inn Red fashion show 2016 kama inavyoonekana pichani.
Mwanadada Wema Sepetu akitoa nasaha zake kwa Wabunifu wa mavazi na wanamitindo (hawapo pichani) wakati wa utamburisho wa jukwaa la Lady In Red fashion show 2016 linalotarajiwa kufanyika 31 Januari.
Martin Kadinda akitoa nasaha zake kwa wabunifu na wanamitindo waliojitokeza katika mkutano huo (hawapo pichani) kuhusiana na jukwaa la Lady In Red fashion show 2016.
No comments:
Post a Comment