Thursday, January 21, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA TAMISEMI MJINI DODOMA LEO

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Georoge Simbachawene akizungungumza kabla ya kukaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzungumza na Wafanyakazi wa TAMISEMI mjini Dodoma Januari 21, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea zawadi ya kikombe kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene ikiwa ni ishara ya Ofisi hiyo kutambua mchango wake wa kuendeleza michezo wakati akiwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo . Mheshimiwa Majaliwa alizungumza na watumishi wa TAMISEMI mjini Dodoma Januari 21, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea zawadi ya kikombe kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene ikiwa ni ishara ya Ofisi hiyo kutambua mchango wake wa kuendeleza michezo wakati akiwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo . Mheshimiwa Majaliwa alizungumza na watumishi wa TAMISEMI mjini Dodoma Januari 21, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa wa TAMISEMI baada ya kuzungumza nao mjini Dodoma Januari 21, 2016.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Benard Makali.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Benard Makali baada ya kuzungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo mjini Dodoma Januari 21, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI , George Simbachawene na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliudi Sanga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI , George Simbachawene baada ya kuzungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo mjini Dodoma Januari 21, 2016. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Benard Makali na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliudi Sanga.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipozungumza nao Ofisini kwake Mjini Dodoma Januari 21, 2016. 
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndiyo kitovu cha nchi na kwamba kila Mtanzania ameelekeza jicho lake pale kwa sababu anasubiri kupata huduma ya msingi.

“Hapa ndiyo kitovu cha nchi na Watanzania wote macho yao yako huku. Kwa nini? Kwa sababu huduma zinasowagusa za barabara, maji, elimu, zinatokea huku kwa maana ya bajeti na usimamizi,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 21, 2016) wakati akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa taasisi na watumishi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwenye mkutano uliofanyika ofisi ya TAMISEMI mjini Dodoma.

“Wananchi wakilalamikia ukosefu wa hizi huduma chanzo ni hapa. Katika wizara kuna mawaziri lakini wao kule ni wasimamizi wakuu. Ninyi chini yenu kuna mikoa, wilaya, halmashauri, rasimali watu na raslimali fedha za kuwasaidia kufikisha huduma tarajiwa kwa Watanzania walio wengi,” alisisitiza.

Waziri Mkuu ameitaka ofisi hiyo ihakikishe inaisimamia vizuri mikoa na halmashauri ili Serikali iweze kupata matokeo mazuri na tarajiwa.

Waziri Mkuu alisema jukumu kubwa lililopo hivi sasa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kuhakikisha kuwa zinabuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya serikali.

“Hatukubaliani na uzembe kwenye idara na halmashauri za wilaya kwa kuwa hivi sasa Serikali ya Awamu ya Tano inasimamia utumishi uliotukuka na wenye uadilifu hivyo kila mmoja ahakikishe anasimamia vizuri eneo lake,” alisema.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kuwahudumia ipasavyo Watanzania wenye uelewa tofauti na matakwa tofauti na kwa kuanzia Serikali imeanza kuwajenga watumishi wa Serikali kutambua kuwa wao ni wahudumu wa wananchi hivyo inawapasa kuwahudumia vema.

“Lazima tujenge moyo wa huruma wa kuwahudumia wenzetu, anapokuja mwananchi msikilize, mhudumie na mwelekeze eneo sahihi ili aweze kupata huduma. Lazima tusimamie na kuona maeneo yote yanafanya kazi kama ilivyokusudiwa, ili kupata matokeo tarajiwa iwe ni wajibu ya kila mmoja kuhakikisha kuwa anatoa usimamizi thabiti katika eneo lake,” alisisitiza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi hao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bw. George Simbachawene alisema TAMISEMI wapo tayari kubadilika na kufanya kazi kama kauli ya Rais John Pombe Magufuli inavyotaka, yaani HAPA KAZI TU.


Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Bernard Makali alimpongeza Waziri Mkuu Majaliwa kwa kusimamia vizuri masuala ya elimu nchini wakati akiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya elimu.

No comments: