Friday, January 15, 2016

WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA SHIRIKA LA TIJA LA TAIFA (NIP)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tija la Taifa (NIP), Novatus S. Massao alilitembelea Shirika hilo Januari 15, 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea Shirika la Tija la Taifa (NIP) Januari 15, 2016.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Tija la Taifa (NIP) wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe.Jenista Mhagama (Mb) hayupo pichani wakati wa ziara yake katika shirika hilo, Januari 15, 2016.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) katikati, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Tija la Taifa (NIP) alipofanya ziara Januari 15, 16 kulia kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Erick Shitindi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tija la Taifa (NIP) Novatus S. Massao (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya NIP Prof. Samwel Wangwe walipokuwa wakiangalia mazingira ya nje ya jengo la Shirika la Tija la Taifa.Januari 15, 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tija la Taifa (NIP) Novatus S. Massao wakati akimonesha chumba cha ofisi ya fedha cha shirika hilo, Januari 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na. Mwandishi Maalum

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ameuagiza uongozi wa Shirika la Tija la Taifa kuwa wabunifu katika utoaji wa elimu kwa umma ili jamii iweze kujua kazi na huduma zinazotolewa na shirika hilo.

Mhe. Mhagama ametoa agizo hilo alipotembelea Shirika la Tija la Taifa (NIP) Januari 15,2016 kwa lengo la kujionea  kazi zinazotekelezwa pamoja na changamoto zinazolikabili shirika hilo.

“Uongozi lazima uangalie changamoto zinazolikabili shirika hili na kuangalia namna ya kugeuza changamoto hizo kuwa fursa muhimu na kutoa elimu kwa umma wa Watanzania ili wajue umuhimu wa kutumia huduma yenu kwa lengo la kujiletea maendeleo,”alisema Mhagama

Waziri alielekeza kuwa lazima viongozi wa NIP wawe wabunifu katika kutumia vyombo mbalimbali vya habari vinavyoweza kuwafikia wananchi wa aina zote huku akisisitiza kuangalia vipindi ambavyo havihitaji kulipiwa.

"Nendeni mkaongee na wadau wa vyombo vya habari maana utakuta kuna fursa nyingi mngeweza kuzitumia bila gharama yoyote. kuna vipindi kama vile Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC 1, kipindi cha Kumekucha cha ITV, kipindi cha 360 Clouds Tv na Tuongee asubuhi cha Star Tv na vingine vingi amabavyo mnaweza kuvitumia kuwafikia wananchi wengi," alisisitiza Mhe. Mhagama.

Waziri alisema kuwa kwa kutumia ubunifu na  fursa zilizoko kwenye vyombo vya habari shirika litapata kujitangaza bila kutumia gharama na kuweza kuyafikia malengo kama kuboresha ujuzi na uelewa wa usimamizi wa  rasilimaliwatu, kuchapisha na kusambaza fasihi na kuboresha utendaji wa Taasisi za umma na zisizokuwa za umma.

Wakati akimkaribisha waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa NIP  Bw.Novatus Massao alieleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazokabili shirika hilo  ni suala la taswira hasi kwa jamii na uelewa mdogo wa jamii kuhusu faida  na umuhimu wa Shirika hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya NIP, Prof.Samwel Wangwe aliahidi kuwa shirika hilo litahakikisha linatekeleza maagizo yote ya Mhe. Mhagama ili kuwezesha watanzania kuelewa na kutumia huduma za shirika hilo.

Aidha, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw.Raphael Loishiye alimshukuru Mhe. Waziri kwa kufanya ziara katika Shirika hilo na kujionea mazingira na changamoto wanazokabiliana katika utekelezaji wa majukumu yao.

No comments: