Friday, January 22, 2016

WAMUOMBA MAGUFULI AWATATULIE TATIZO LA KIWANDA CHA MAFUTA KINACHO WACHAFULIA MAZINGIRA

 Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa anaongea na wananchi wa eneo la Mbauda lililopo ndani ya jiji la Arusha

Na Woinde Shizza,Arusha

Msafara wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli   uliokuwa ukielekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli  mapema leo umesimamishwa na wananchi  katika eneo la Mbauda lililopo ndani ya jiji la Arusha  ili kushinikiza kutatua kero zao na changamoto zao ikiwemo kuwepo na  kiwanda cha mafuta  ya kupikia cha  Mount Meru   Mill  kinachodaiwa kuchafua mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo.
Wananchi hao ambao walijikusanya kuanzia mida ya saa mbili kamili asubui mbali na kumueleza Rais huyo kero zao, pia walitumia nafasi hiyo kumpongeza kwa kazi anayofanya na kumuomba aendelee kutumbua majipu yaliyopo  humu nchini.
Akiongea mbele ya Rais mara baada ya kupewa nafasi , mmoja wa wanachi wa eneo hilo la mbauda  Thabiti Abubakari alimuomba rais awasaidie kutatua tatizo la kiwanda hicho kutiririsha maji machafu ya kiwandani  kwani tatizo hilo ni baya na linawaharibia mazingira  na kuhatarisha afya zao.
‘’Musheshimiwa Rais tunapenda utusaidie hapa kwetu mbauda tuna kero kubwa inatusumbua, kuna hiki kiwanda cha mafuta ya kupikia cha mount meru mill kimekuwa kinatiririsha maji machafu ya kiwandani huku nje ambapo wananchi wanaishi  , kiwanda hiki  hakijajenga mitaro  ya kupitisha maji machafu hivyo maji yote machafu yakitoka huko kiwandani yanaingia huku majumbani kwetu, hivyo muheshimiwa tunaomba utusaidie hili tatizo kwani kiwanda hiki kipo ndani ya makazi ya watu,kinahatarisha afya  sasa inatuatarishia afya zetu pamoja na za watoto wetu ambao wanacheza uku mitaani pia tunaweza kupata magonjwa ya milipuko kama kipindupindu maana maji haya ni machafu sana”alisema Dhabiti

Akijibu swala hilo Rais magufuli alisema kuwa amelisikia na aliwaagiza mamlaka ya usafi wa mazingira  NEMC   kulifuatilia swala hili mara moja .
Aidha Rais Magufuli alitumia muda huo kuwashukuru wananchi wa jiji la Arusha kwa jinsi walivyoendelea kujitokieza kumpokea na kuwaahidi kuwa ataendelea kutekeleza yale yote aliyoyahaidi katika kipindi alipokuwa akifanya kampeni.
Alisema kuwa kipindi hiki hakuja Arusha kwa ajili ya kuongea na wananchi hivyo basi ataandaa siku na kuja rasmi Arusha kufanya mkutano mkubwa ambao pia atatumia muda huo kusikiliza kero za wananchi wa jiji la hilo.

No comments: