Tuesday, January 19, 2016

TATIZO LA KANSA YA SHINGO KIZAZI NI KUBWA KULIKO YA WANAOTOA HUDUMA HIYO.

Meneja wa Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi wa UMMATI, Jeremiah Makula akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kanda Kusini Mwa Afrika, Ulla Muller akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Neema Rusibamayilla akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wakurugenzi wa Mashirika yaliyokuwa na Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi pamoja na wawakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifatilia maada wakati wa mkutano wa utoaji wa tunzo kwa wadau wa mradi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wakifatilia maada wakati wa utoaji tunzo kwa mashirika yaliyokuwa katika mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii). 

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii 
WADAU wa wanaoshughulika na kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake ni wachache ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo nchini kwa tatizo hilo. 

Akizungumza katika mkutano wa wadau waliokuwa wakifanya Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi na Kinga kwa wanawake dhidi ya kansa hiyo, Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Neema Rusibamayilla amesema serikali inatambua juhudi za wadau ambao wamekuwa wakifanyia wanawake juu ya kinga ya kansa ya shingo ya kizazi. 

Amesema serikali itaendelea kushirikiana wadau mbalimbali katika kukabili tatizo la kansa ya kizazi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wanawake kujitokeza kupima afya zao na inapotokea na tatizo hilo kushughulikiwa kwa haraka. 

Neema amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa pale inapohitajika katika kukabili tatizo la kansa ya shingo ya kizazi kutokana na serikali peke yake haiwezi kushugulikia matatizo kwa wakati mmoja. 

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa UMATI, Lulu Ng’wanakilala amesema kansa ya kansa ya shingo ya kizazi inaua hivyo ni lazima wanawake kupima mara kwa mara kabla tatizo halijawa kuwa kubwa. 

Amesema wadau wanaoshughulika na kansa hiyo ni wauchache ikilinanishwa na tatizo lilopo hasa katika maeneo ya vijijini ya kuwa na wanawake wengi ambao hawajafikiwa kwa kupima au kupata huduma hiyo. 

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes ,Anil Tambay akiwakilisha wadau walikuwa katika mradi huo amesema mafanikio walioyapata katika mradi huo ni kwa kusaidia wanawake uhai katika utoaji wa tiba ya kansa ya shingo ya kizazi.

1 comment:

Anonymous said...

Hongereni sana wadau wote wa kusaidia kupambana na kansa ya shingo ya kizazi. mgodi wa STAMIGOLD uliopo wilayani biharamulo ulifanikiwa kufanya uchunguzi kwa kina mama zaidi ya 300 waishio vijiji viivyo jirani na mgodi kupitia UMATI kanda ya Mwanza. awareness hasa vijijini bado ni ndogo sana na wengi wana imani potufu kuwa unavyopimwa unafungwa kizazi hivyo hutoweza kuzaa tena. tuendelee kushirikiana kuta elimu zaidi vijijini ili kuleta uelewa na kuokoa vifo visivyo vya lazima.