Thursday, January 21, 2016

SSRA kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii

Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka (katikati), akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi na kulia ni Ofisa Uhusiano wa SSRA, Agnes Lubuva. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. 
Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka (katikati), akitoa taarifa kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Baadhi ya wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua picha na taarifa iliyokuwa ikitolewa na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakisikiliza na kuchukua taarifa iliyokuwa ikitolewa na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakichukua maswali ya waandishi wa habari, walipokuwa wakitaka ufafanuzi kuhusu mamlaka na mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii nchini.
Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mamlaka hiyo pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii. Katikati ni Ofisa Tehama wa SSRA, Ernest Masaka na kulia ni Ofisa Uhusiano wa SSRA, Agnes Lubuva.
Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi (kushoto), akijibu maswali ya waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mamlaka hiyo pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii. 


Na Mwandishi wetu

MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema imeanzisha utaratibu mpya wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).
Ofisa wa Tehama wa mamlaka hiyo, Ernesti Masaka amesema hayo, leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.
Alisema kuwa kwa sasa mwanachama yoyote mwenye malalamiko kuhusu huduma za mifuko ya hifadhi ya jamii au maoni yake mbalimbali anaweza kufanya mawasiliano na mamlaka kwa urahisi kupitia njia ya kieletroniki  inayopatikana kwa watumiaji wa simu za mkononi na kwenye simu hizo huduma hiyo inapatikana kwenye Google play kwa jina la SSRA.
"Mlalamikaji pia anaweza kutuma malalamiko yake kupitia kwenye tovuti ya mamlaka ya www.ssra.go.tz na kwenda sehemu iliyoandikwa malalamiko na maoni. Uanzishwaji wa mfumo huo ni moja ya hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii namba 8 ya mwaka 2008 iliyoboreshwa kwa sheria namba 5 ya mwaka  2012 alisema".
Aliongeza utaratibu huo umeanzishwa ili kurahisishia mwanachama yoyote kutoa malalamiko yake kuhusu masuala ya sekta hiyo ambapo anaweza kufanya hivyo akiwa mahali popote.
Alisema mwanachama yoyote anaweza kupakua mfumo wa malalamiko kwenye simu yake kupitia google play  kwenye simu yake na kuanza kutuma malalamiko yake au kupitia kurasa ya kwanza ya tovuti ya mamlaka.

Ambapo ataweza kuingia katika mfumo huo wa malalamiko na maooni na utampeleka moja kwa moja katika kurasa itakayomuwezesha kuingiza taarifa binafsi za mwanachama mwenye lalamiko kwa ajili ya kushughulikia malalamiko ya wanachama.
"Mfumo huu wa malalamiko umezingatia uwekaji mzuri wa kumbukumbu kwa upande wa mamlaka ambapo huonesha ripoti kwa ufupi za jumla ya malalamiko yanayoendelea  kufanyiwa kazi, yaliyokamilika kufanyiwa kazi na mfuko husika wenye malalamiko hayo.
Pia  mfumo huo hutoa taarifa za malalamiko ya wanachama kwa vigezo vya aina ya malalamiko kwa idadi na hatua ya utekelezaji  iliyofikiwa,"alisema Masaka.Aliongeza kwa ujumla mawasiliano kati ya wananchi na mamlaka yameimarishwa kwa matumizi ya simu za mkononi kwa njia ambazo zimeorodheshwa hapo juu.Pia mamlaka hiyo ina utaratibu wa kuwasiliana na wadau kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu na barua pepe.

No comments: