Thursday, January 7, 2016

SKULI YA MSINGI YA ZINGWEZINGWE YAZINDULIWA ZANZIBAR.

G2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman akikunjuwa kitambaa ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya  Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
G1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya Zingwezingwe.Ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya  miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
G6
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya  Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja,Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kushoto ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Juma Kassim Tendwa.

G3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman akipanda mti wa Mnazi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira katika Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya  Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
G4
Baadhi ya Walimu pamoja na wanafunzi waliohudhuria katika Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya  Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
G5
Wanafunzi Khadija Khamis kushoto na Asha Mahamudi kutoka Skuli ya Fujoni wakisoma Utenzi katika Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya  Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Na Ali Issa Maelezo –Zanzibar 
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haruon Ali Suleiman ameshauri  walimu watakaosomesha Skuli ya Zingwezingwe wawe walimu wanaoishi karibu na  kijiji hicho.

Hayo ameyasema leo huko Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, wakati alipokuwa akifungua skuli mpya ya msingi ya kijiji hicho ikiwa ni miongoni mwa  shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .

Ametaka ushauri huo ufanyiwe kazi  na iwapo watahitajika walimu wapya  kuajiriwa kwa  ajili ya kufundisha katika skuli hiyo  Wizara yake   ambayo ndiyo  inayohusika na  masuala ya ajira   watakuwa tayari  kufanya hivyo.

“Ni vyema kuajiri walimu wakaazi  na wenyeji wa kijiji cha Zingwezingwe  wenye kuyaelewa mazingira ya kijiji hicho na mimi kama Waziri wa Ajira niko tayari   kusaidia hilo,” alisema Waziri Haroun.Aidha aliwashauri wanafunzi  wanaosoma  katika skuli hiyo  kuitumia  frusa waliyoipata  kusoma kwa juhudi  kwani hiyo ni skuli ya kwanza  kujengwa katika kijiji hicho.

Hata hivyo aliwataka wazazi  na walezi kwa  upande wao kutimiza wajibu wao  wa kufuatilia kikamilifu maendeleo ya Watoto  wao  na kutoa ushirikiano  kwa walimu ili kufanikisha maendeleo ya watoto wao.Waziri Haroun  aliwataka walimu kusomesha kwa juhudi kwani serikali  tayari imeshatoa maelekezo ya kuwaongezea maslahi yao  mara itakaporudi madarakani baada ya uchaguzi  wa marejeo.

Katika kuongeza ujenzi wa madarasa mengine ya kusomea katika Skuli hiyo, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utawala wa Umma  alichangia matofali 1000 ambapo ujenzi wake utaaza hivi karibuni.Nae Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Mama Asha Balozi akitoa salamu za Baloz Seif Ali Idd alisema suala la umeme katika skuli hiyo litafanywa na Makamu huyo wa Rais.

 Ujenzi wa skuli hiyo yenye  madarasa  manne na Ofisi ya Mwalimu Mkuu umegharimu shilingi milioni 66 ambazo zimetolewa na  Shirika la Maendeleo la Sweden SIDA, Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B, Mbunge na Mwakilishi na Wazee wa kijii cha Zingwezingwe.

No comments: