Saturday, January 23, 2016

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI January 22, 2016.

Shirikisho la soka TFF limetima salamu za rambirambi kwa klabu ya Prisons FC kufuatia kifo cha mwenyekiti wake Hassan Mlilo. https://youtu.be/kO7Rq-3uU48
  
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salim Jecha ametangaza kuwa uchaguzi visiwani humo utafanyika tarehe 20 mwezi wa 3.   https://youtu.be/3XKNsH8WyvI

Rais Magufuli atanabaisha mchango wa jeshi la wananchi katika kuleta maendeleo ya jamii ya watanzania.   https://youtu.be/_dkAD9V0Wn4

Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya ndege ya Tanzania amesema watahakikisha wanaleta ushindani katika huduma ya usafiri wa ndege ndani na nje ya nchi.   https://youtu.be/4fNOIPsZsIQ

Tathmini ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2015 umebaini kuwa uchaguzi huo ulikuwa ni wa huru na haki katika nyanja zote kuanzia kampeni hadi utolewaji wa matokeo. https://youtu.be/v8Yuh6DhWoQ   

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage ameitaka kamati ya kusimamia kesi ya kiwanda cha Urafiki kuiomba mahakama kuiendesha kwa haraka ili kuepusha migomo ya wafanyakazi.   https://youtu.be/772WCHeoLiE

Makamu wa rais wa shirika la riadha duniani amesifu maandalizi ya riadha ya Tokyo yanaoendelea kufanyika nchini Japan. https://youtu.be/wFb03TosbPE

Waziri wa ujenzi Prof. Makame Mbarawa awasimamisha watumishi wanne wa mamlaka ya bandari mkoani Mwanza; https://youtu.be/kh8bNfWzHVs

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda awataka  wananchi kujitokeza kwa wingi katika huduma ya bure ya  uchunguzi ya afya ya moyo https://youtu.be/NgRvLQ8K6AI

Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein awaongoza wananchi wa Zanzibar katika mazishi ya marehemu Asha bakari; https://youtu.be/K85tdjLT2Ec

Watanzania washauriwa kutumia mboga za majani pamoja na matunda kwa afya borahttps://youtu.be/Z5KsJ7k742Y

Kamati ya shindano la urembo Tanzania yaamua kujindoa katika kuandaa shindano hilo; https://youtu.be/FyfEqI1UIl8

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Congo DRC yafanikiwa kuigia hatua ya robo fainali ya michuano ya CHAN inayoendelea nchini Rwanda; http://zantel.tv/2cyi7oO

Mchezaji wa kimataifa toka nchini Rwanda, Haruna Niyonzima aanza rasmi mazoezi na timu yake Yanga; https://youtu.be/Ukmy-rMi1yA

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi visiwani Zanzibar, Jecha Salim Jecha atangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi wa Zanzibar; https://youtu.be/VGipmvltJ40

Rais John Magufuli aiagaiza wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa kuimarisha kikosi cha Nyumbu ili kukidhi malengo ya kuanzishwa kwake;https://youtu.be/Onuc2fPQG48

Waziri wa nishati na madini Prof. Peter Muhongo awakaribisha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya umeme; https://youtu.be/AUzK465Caqo

Mkuu wa mkoa wa Kagera ameunda timu ya watu watano kuchunguza tuhuma ya ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa barabara katika halmshauri ya wilaya ya Bukoba;https://youtu.be/U0WPBM8ZcvE

Mkuu wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara apiga marufuku kwa wakulima wa zao la Korosho kukatwa pesa kuchangia mfuko wa bima ya afya;https://youtu.be/HokJVhd2C9Y

Kampuni ya simu za mkonoini ya Zantel yatoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununua vifaa vya kufundishia katika shule ya watoto wenye ulemavu ya Kisiwandui iliyoko Unguja; https://youtu.be/gYuQUISlkJ0

Kocha mkuu wa timu ya Prison awaakikishia mashabiki wa mpira mkoani Mbeya kuwa timu ya Prisons itafanya vizuri mzunguko wa pili; http://zantel.tv/Y3FoH7I

No comments: