Wednesday, January 6, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Serikali yapinga mapendekezo ya nauli ya mabasi yaendayo haraka iliyokuwa imependekezwa na wamiliki wa mabasi hayo; https://youtu.be/F4DoFZZOZPo  

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi meneja wa kiwanda cha kusindika Tumbaku cha SONAMCU mkoani Ruvuma kwa tuhuma za ubadhilifu;https://youtu.be/bE_iEHagLdk  

Hali ya sintofahamu imetanda kwa wakazi wa Bukoba kufuatia Meli ya MV.Serengeti iliyokuwa ikitoka Mwanza kwenda Bukoba kupata hitilafu ikiwa safarini; https://youtu.be/gCukCZx5HGI  

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeanza kuzindua miradi yake mbalimbali ya maendeleo katika kuelekea maadhimisho ya miaka 52 ya mapinduzi;https://youtu.be/MN_RNuyHz3U  

Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/3nqCin9dokc  

Mamlaka ya mapato nchini TRA imevuka lengo la makusanyo ya kodi kwa mwezi wa 12 mwaka 2015 kwa kukusanya jumla ya shilingi trioni 1.4;https://youtu.be/t_grkb1mqT4  

Serikali imeiagiza bodi ya utalii nchini kuvitangaza vivutio vya utalii nchini katika vyombo ya habari vya kimatifa kwa lengo la kupata watalii wengi;https://youtu.be/eCa-RhNJI4c  

Michuano ya kombe la shirikisho kwa mzunguko wa tatu inatarajiwa kuanza mwezi huu huku ikianza kushirikisha timu za ligi kuu;https://youtu.be/Sc_Hvvvl3Ww  

Zaidi ya abiria 52 wamenusurika kufa katika ajali ya basi iliyotokea wilayani Nzega mkoani Tabora; https://youtu.be/EDEkBK9TZmU  

Baadhi ya wananchi wa Simanjiro mkoani Manyara wamedaiwa kuvamia mgodi wa Tanzanite Mererani kupinga kitendo cha mgodi huo kupunguza wafanyakazi; https://youtu.be/nvXBbFR_svg  

Watumishi 9 wa manispaa ya Kigoma Ujiji wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma; https://youtu.be/t_mpFk1QcJg  

Serikali imewataka wananchi wasiohusika na zuio la mahakama la kusitisha bomoabomoa kuanza kuondoka wenyewe; https://youtu.be/x-sjzqXIHxQ   

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Iringa wanakabiliwa na changamoto ya huduma za afya kutokana na kukwama kwa ujenzi wa zahanati iliyosababishwa na mvua za mawe; https://youtu.be/6tK4JbwIMZM  

Waziri wa viwanda Charles Mwijage amesema serikali imejipanga kuhakikisha bei ya sukari nchini inakuwa si kandamizi kwa wananchi;https://youtu.be/FWysKhcTLVo  

Mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samata amepewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora afrika kwa wachezaji wa ndani ya Afrika;https://youtu.be/3rxdRW51YQ4  

Timu ya taifa ya Zambia imetangaza kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya CHAN nchini Rwanda; https://youtu.be/zEbGddCgzhc  

Hatimaye takataka zilizokuwa zimerundikwa katika eneo la Keko jijini Dar es salaam zaondolewa kufuatia agizo la mkuu wa mkoa huo.https://youtu.be/vhyy0nTXsgw   

Makamu wa rais Bi.Samia Suluhu awataka maafisa misitu kote nchini kuacha mara moja kuhamisha wananchi wanaodaiwa kuvamia misitu pamoja na kufyeka mazao yao. https://youtu.be/R-ZlXS9B2mg

Rais wa Zanzibar Dr.Shein awataka madaktari na wauguzi wote visiwani humo kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa viapo vyao vya kazi.https://youtu.be/-Q9HK4YQkDc

Baadhi ya wakazi wa kata ya Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wavamia eneo la mgondi wa Tanzanite na kusababisha uharibifu wa miundombinu ikiwemo bomba la maji. https://youtu.be/hbo4cSVXXTc

Treni ya abiria inayofanya safari zake kutoka katikati ya jiji kwenda Ubungo jijini Dar es salaam yashindwa kufanya safari zake na kusababisha adha kwa wananchi baada ya wafanyakazi wake kugoma.  https://youtu.be/bK5gPm1ujKs

Waziri mkuu Kassim Majaliwa apinga vikali viwango vya nauli za mabasi ya mwendokasi vilivyopendekezwa huku akitoa maagizo.https://youtu.be/zHQMo-fJC9o

Mamlaka ya mapato nchini TRA yaendelea na ukusanyaji wa mapato ya serikali kutoka kwa makampuni yaliyokwepa kodi huku ikibainisha kukusanya takribani shilingi bilioni 11. https://youtu.be/IEABWv6Y2yc

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi aiagiza idara ya uhamiaji mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha inadhibiti wahamiaji haramu nchini.https://youtu.be/cS8cMHS4hEc

Mgogoro wa CHADEMA mkoani Rukwa waendelea kufukuta huku baadhi ya wananchama wake wakichukua maamuzi ya kuchagua viongozi wapya.https://youtu.be/V0KLwkTH-30

Jumuiya za dini ya Kiislamu huko Zanzibar zaingilia kati mgogoro wa kisiasa visiwani humo huku zikitaka ufumbuzi wa haraka.https://youtu.be/Woq2Mxq0EeY

Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kigoma imetangaza rasmi kuwasimamisha kazi kwa muda usiojulikana jumla ya watumishi 9 kwa tuhuma za ubadhilifu.https://youtu.be/qO1qnG1Y3s8

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mwigulu Nchemba awafukuza kazi viongozi wa vyama vya msingi na ushirika vya wakulima wa tumbaku mkoani Iringa. https://youtu.be/uO5Z-zdDSik

Hekari 10 za mazao ya mahindi, miwa na migomba mali za wananchi mkoani Njombe zimefyekwa na askari wa pori la akiba la Mpanga Kipengele.https://youtu.be/qo58rJjwdFg

Familia ya mjane mmoja mkoani Mwanza yajikuta katika wakati mgumu kufuatia nyumba iliyokuwa ikiishi kubomolewa na dalali wa mahakama kufuatia kuuziwa eneo hilo kinyume cha sheria. https://youtu.be/EGXk80sHONI

No comments: