Tuesday, January 12, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu muungano na mazingira aiagiza NEMC na halmashauri ya jiji la Mwanza kubaini waliojenga mabondeni.https://youtu.be/x82pObwHrXc
Zaidi ya wakazi 28 waliosahaulika kwenye ulipaji wa fidia kwenye maeneo yalichukuliwa na TPDC kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea waililia serikali. https://youtu.be/lmopqyO9HxU

Wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya waiomba serikali kuwajengea daraja kufuatia daraja lilipo hivi sasa kuwa hatarishi kwa maisha yao.https://youtu.be/m53NYXE0aaQ

Serikali ya Tanzania imekarbisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme na viwanda baada ya kupata zaida ya gesi asilia futi za ujazo zaidi ya milioni 100 kwa siku. https://youtu.be/eL-HoHkUKSo

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamekuwa na maoni tofauti juu ya maadhimisho ya sikukuu ya mapinduzi Zanzibar huku wakitoa rai kusuluhisha mgogoro uliopo Zanzibar. https://youtu.be/tncMN_QKwXM

Rais Dkt. Ali Mohammed Shein  aongoza watanzania katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 52 ya mapinduzi ya Zanzibar;https://youtu.be/yWtPWfip3II

Wananchi mkoani Tabora waadhimisha miaka 52 ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kufanya usafi wa mazingira mkoani humo; https://youtu.be/WkmOwGLIFh4

Mkazi mmoja wa Iringa amefariki kwa kuangikiwa na ukuta wa nyumba na mwingine kunusurika kifo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo;https://youtu.be/yIBKB9jJaMY

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe.Ummy Mwalimu avipandisha hadhi vituo viwili vya afya vilivyopo wilayani Songea mkoani Ruvuma; https://youtu.be/hHbvQGeDkGM

Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam yamfuta kazi kocha mkuu, Dylan Kerr pamoja na benchi zima la ufundi; https://youtu.be/VyAQ7BTTQgs

Mshambuliaji Mbwana Samata asema inahitajika mipango maalum katika kuiboresha timu ya taifa ya Taifa Stars; https://youtu.be/klbm-OtRsYU

Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein awahimiza wananchi kuendelea kudumisha amani visiwani humo; https://youtu.be/9ve4vVHLvVQ

Serikali yaifutia leseni kampuni ya wakala wa ajira ya Salama Investment Limited iliyoko mkoani Mwanza kwa kukiuka sheria ya ajira nchini;https://youtu.be/M65DsD-TqrI

Serikali yawatoa hofu wananchi wa Gongo la mboto kuhusu zoezi la bomoabomoa inayoendelea jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/zvJ_xAdvlqA

Baadhi ya wakazi wa Shinyanga wamejikuta katika wakati mgumu baada ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo kuharibu miundombinu;https://youtu.be/46_d4zpA8sc

Halmashauri ya wilaya ya Nzega yafunga maduka 400 kwa madai ya wamiliki wa maduka hayo kukaidi kulipa kodi; https://youtu.be/VX-UrxkiIP4

Timu ya Coastal Union ya Tanga yamtangaza kocha Ali Jangalu kuwa mrithi wa Jackson Mayanja aliyejiunga na timu ya Simba; https://youtu.be/wjO67lh26OU

Kocha Louis Van Gaal ajitetea kuhusu mashabiki kuwahi kuondoka uwanjani wakati wa mchezo baina ya Manchester United na Sheffield United wiki iliyopita; https://youtu.be/WZQY2MHEh2w

No comments: