Wednesday, January 6, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein awataka wahudumu wa afya visiwani humo kuzingatia maadili ya kazi yao; https://youtu.be/fPzwcfOhhG0  

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amuagiza katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati mkoani humo;https://youtu.be/dQuDOSDEj7Q

Mkutano wa kujadili mapendekezo ya nauli mpya za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam umeanza kwa wadau mbalimbali kukutana kujadili mapendekezo hayo; https://youtu.be/DQ_4BdMhv2A  

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za kibenki nchini kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wananchi wenye vipato vya chini;https://youtu.be/chPixMM0HnE  

Naibu waziri wa nyumba, ardhi na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula ameishauri kampuni ya ujenzi wa nyumba ya watumishi Housing kujenga nyumba vijijini kwa ajili ya watumishi wa umma;https://youtu.be/9_r3tunKNy8  

Shirikisho la mpira wa miguu TFF limesema liko tayari kuchunguzwa ikiwa watu wanashaka na kuwepo kwa rushwa ndani ya shirikisho hilo;https://youtu.be/BSOE40SxlCo  

Mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samatta anatarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Nigeria kuhudhuria tuzo za mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani ya bara la Afrika; https://youtu.be/nT7vpES4AbM    

Mahakama Kuu ya Tanzania kitengo cha ardhi yaiamuru serikali kusitisha zoezi  la bomoabomoa  kwa wakazi wa mabondeni kwa muda;https://youtu.be/QvC8CcGQTfU  


Hatimaye serikali imefanikiwa kumaliza mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 10 baina ya wananchi na mwekezaji wa shamba la Kapunga mkoani Mbeya;https://youtu.be/nE4xE3_Bo4M  

Jeshi la polisi mkoani Singida limefanikiwa kumkamata kijana mmoja  kwa tuhuma za ujambazi sugu; https://youtu.be/RLoV1MbRxEI   

Wafanyakazi zaidi ya miamoja wa kiwanda cha vyombo cha Cello kilichopo Dar es Salaam wameendesha mgomo kushindikiza kulipwa stahiki zao;https://youtu.be/D-n_nsvmhPA  

Mgodi wa dhahabu wa Geita kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya mji wa Geita kwa pamoja wametekeleza mradi mkubwa wa kisasa wa ushonaji wenye lengo la kuinua uchumi kwa wakazi wa Geita; https://youtu.be/KCUEYQWvY9k  

Kocha wa timu ya Jamhuri kutoka visiwani Zanzibar amesema timu yake imejiandaa kupambana na sio kushiriki; https://youtu.be/i08hecyuuOI  

Wasanii wa muziki nchini wako katika sintofahamu kuhusu tamko la serikali kutaka vyombo vya habari kuwalipa wasanii kwa kucheza kazi zao;https://youtu.be/K3TCRoB5XkA   

Uongozi wa klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania imemtambulisha Zinedine Zidane kama kocha mkuu wa klabu hiyo; https://youtu.be/QtgTnUNv-fE 
 

Zoezi la bomoa bomoa kwa wakazi wa mabondeni na maeneo ya wazi laendelea jijini Dar es salaam baada ya kusimama kwa muda.https://youtu.be/yx7gyjXLPjc  

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi yaiagiza idara ya uhamiaji nchini kuanza operesheni maalum ya kuwabaini wageni wanaofanya kazi nchini ambazo zinaweza kufanywa na watanzania. https://youtu.be/BK_rwttD1IE  

Mahakama kuu kitengo cha ardhi kanda ya Dar es salaam yaagiza kusitishwa kwa zoezi la bomoabomoa katika maeneo ya mabondeni kwa wamiliki walioomba kupitia shauri namba 822 la mwaka 2015 mpaka hapo litakaposikilizwa siku ya juma tatu. https://youtu.be/P6Nur8wVMrU  

Makamu wa Raisi Bi.Samia Suluhu azindua mradi wa maji uliojengwa na kampuni GGM inayofanya shughuli za uchimbaji mkoani humo.https://youtu.be/vStpo3nsiLs   

Serikali yasema inakusudia kufuta hati miliki ya za mashamba ya wawekezaji walioshindwa kuyaendeleza kwa muda wa miaka 10 na zaidi.http://simu.tv/prEoaJ2
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aagiza mamlaka zinazohusika kuondoa mara moja taka zilizorundikwa eneo la Keko kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi. https://youtu.be/qA6XddQTB4o  

Mahakama kuu kitengo cha ardhi yazuia zoezi la bomoa bomoa kwa nyumba 674 wilayani Kinondoni hadi pale hukumu itakapo tolewa.https://youtu.be/q7g7zUvc-t4  

Waziri mkuu amuagiza mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma kuondoa mara moja duka lake la dawa lililopo pembezoni mwa hospitali ya mkoa.https://youtu.be/7-_tG0yYYMQ   

Waziri wa maliasili na utalii aanza kutumbua majipu huku akimsimamisha kazi mkurugenzi wa mipango na matumizi wa wizara hipo.https://youtu.be/2G8F5M4H-Gk  

Zaidi ya kaya 2778 wilayani Kilosa mkoani Morogoro hazina mahala pa kuishi kufuatia makazi yao kuharibiwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha. https://youtu.be/h0-8naELpp0  

Mbunge wa jimbo la Segerea mh.Bonnah Karua atoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa darasa la kwanza jimboni humo.https://youtu.be/IovM21DCTbg  

Wadau wa usafiri wageuka mbogo na kupinga vikali nauli za mabasi ya mwendo wa haraka zilizo pendekezwa na watoaji wa huduma wakidai haziendani na maisha ya mtanzania wa kawaida. https://youtu.be/GI0jhOSCclg  

Raisi wa Zanzibar Dr.Shein azindua ujenzi wa jengo la hospitali ya Mnazi Mmoja litakalotumika kuhudumia wakina mama na watoto.https://youtu.be/mupLu6ksuAo

Jumla ya wanafunzi 9000 wa darasa la awali na wale wa darasa la kwanza waanza kunufaika na mpango wa elimu bure. https://youtu.be/nXCF2PA1bJ0

No comments: