Saturday, January 16, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Baraza la mitihani la taifa NECTA latangaza matokeo ya kidato cha 2 huku mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kutoa shule ya 1 na 2. https://youtu.be/JLyzB4ttJ08 

Wananchi wa kijiji cha Mahanje wilaya ya Madaba waikataa kampuni ya kufua umeme ya Mkonge Energy System kufuatia mgogoro wa ardhi.https://youtu.be/a0f-U_eCXkY  

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof.Makame Mbarawa pamoja na waziri wa fedha wamsimamisha kazi kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga pamoja na wafanyakazi wengine wa shirika hilo.https://youtu.be/RLWfjftfgs8   

Mkazi mmoja wa Kilimanjaro yuko hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kufuatia kuishi kwenye mazingira hatarishi. https://youtu.be/04HtwglG8FA   

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano azifungia radio 28 nchini kwa kosa la kutolipia ada za leseni zao. https://youtu.be/BiY01SC8Xew  

Waziri wa afya apiga marufuku kwa vyombo vya habari nchini kupiga matangazo ya tiba asili kwani yaliyo mengi hayajasajiliwa.https://youtu.be/fzqsF-BSq3Y  

Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki zatakiwa kupiga marufuku uingizwaji wa silaha nchini Burundi huku Tanzania ikinyooshewa kidole.https://youtu.be/8ruWexXToD0  

Wananchi wilayani Serengeti waiomba wizara ya ardhi pamoja na wizara ya maliasili kuutaftia ufumbuzi mgogoro wa mapaka kati ya wananchi hao na pori la akiba la Ikorongo. https://youtu.be/hSiOmO6b0Ks  

Meli ya Mv.Serengeti inayofanya kazi zake kati ya mikoa ya Mwanza na Kagera yarejea safari zake zilizositishwa hapo awali kufuatia hitilafu katika injini.https://youtu.be/5vFzMVJg80U  

Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga, asimamishwa kazi kwa tuhuma za kukiuka sheria ya manunuzi ya umma;https://youtu.be/yfnDdvjIkF8  

Kamati ya kanuni za bunge iliyoundwa na Spika Job Ndugai yakutana na kujadili mapendekezo yaliyotolewa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai;https://youtu.be/N5NT8m5ST9I   

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, Mhe. Jenista Mhagama amuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuchunguza fedha zilizotolewa kwa shirika la tija la taifa NIP; https://youtu.be/fvmA3Bh8cF8  

Halmshauri ya jiji la Tanga yatakiwa kuwafikisha mahakamani watumishi wa ardhi watakaobainika kuuza kiwanja kwa mtu zaidi ya mmoja;https://youtu.be/aFhkeXWO48w  

Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo nchini wameiomba serikali kuangalia upya utaratibu wa kukata leseni kila mwaka;https://youtu.be/pCbHEWyJyX4  

Serikali yauagiza uongozi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi kuhakikisha mradi huo wa mabasi yaendayo haraka unaanza kutekeleza majukumu yake haraka; https://youtu.be/t9EjZn3-_Mg  

Ligi kuu soka Tanzania bara inatarajiwa kuendelea jumamosi hii katika viwanja tofauti huku mchezo baina ya Simba na Mtibwa Sugar katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ukitegemewa kuvuta hisia za wapenda soka wengi;https://youtu.be/t9EjZn3-_Mg  

Wananchi wa Burundi wametakiwa kuoandoa tofauti zao kwa lengo la kurudisha amani ndani ya taifa hilo; https://youtu.be/buF_ysgNgwU   

Baraza la mtihani Tanzania NECTA latangaza matokeo ya mtihani wa mchujo kwa wanafunzi wa kidato cha pili; https://youtu.be/Ls-9jrmE8e4   

Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo aagiza kukwamatwa kwa vifaa vya mwekezaji wa uchimbaji madini ya makaa ya mawe mkoani Mbeya kwa tuhuma ya uchimbaji madini kinyume na sheria; https://youtu.be/g-Ib5YMBlS  

Serikali yakifunga kiwanda cha uchakataji nyama cha Xing Xua kilichopo wilayani Kahama kwa tuhuma za kukiuka sheria za uendeshaji wa viwanda nchini; https://youtu.be/RH82CO4SzQg  

Wafanyabiashara mjini Babati, wagoma kuuzia bidhaa zao ndani ya soko jipya kwa madai kwamba soko hilo limejengwa chini ya kiwango;https://youtu.be/nzX7mdGz6YM  

Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji nchini EWURA yapunguza kiwango cha uchakachuaji wa nishati ya mafuta kutoka kiwango cha asilimia 78 hadi asilimia 7; https://youtu.be/YWCb48sdukk  

Michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika inatazamiwa kutimua vumbi jumamosi hii nchini Rwanda;https://youtu.be/kBdy60CkkXY

Kocha mkuu wa klabu ya Mtibwa Sugar Meck Mexime amesema licha ya Simba kumtimua kocha wake, bado mchezo wao dhidi ya Simba utakaofanyika jumamosi hii utakuwa mgumu; https://youtu.be/3b--bGI76V0

No comments: