Thursday, January 14, 2016

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA HABARI AKIWA ZIARANI RUFIJI.

 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura akiongea na watumishi wa Wilaya ya Mkuranga wakati ya ziar ya kujionea shughuli za maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilayani humo, wa pili kutoka kulia na Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdala Ulege na wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Abdalla Kihato.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura wa pili kutoka kulia akipokea taarifa ya utekelezaji wa kikundi cha Sanaa za maigizo kilichopo wilaya ya Rufiji Bw. Bashiru Kibopo wakati ya ziara ya kujionea shughuli za maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilayani humo,wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo hilo Mh. Allyseif Ungando na wa kwanza kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Rufiji Bi. Maria Katemana. 
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura aliyenyoosha mkono akiongea na baadhi ya wasanii waliojenga katika kijiji cha Wasanii na wanahabari kilichopo Wilayani Mkuranga wakati ya ziara aliyofanya ya kujionea shughuli za maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilayani humo. 
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura (mbele) akiongea na wakazi wa Wilaya ya Mkuranga katika uwanja wa wilaya hiyo uliojengwa kwa nguvu za Serikali ya mtaa na nguvu ya wananchi uliogharimu shilingi milioni sabini na mbili.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdalla Ulege akiongea na wakazi wa jimbo lake wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura ya kujionea shuguli za maendeleo ya sekta hiyo. 
Mwenyekiti wa mtandao wa wasanii (SHIWATA) Bw. Cassim Talib katikati akimuonyesha baadhi ya nyumba za wasanii na wanahabari zilizopo Wilayani humo Mh. Anastazia Wambura wa kwanza kushoto wakati ya ziara ya kujionea shughuli za maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilayani humo., kulia ni msanii wa sanaa za maigizo maarufu kama mzee Chilo. 
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura akisalimiana na Mbunge wa Rufiji Mh. Allyseifu Ungando wakati wa ziara ya kujionea maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wilayani humo.
 (Picha na Benjamin Sawe- WHUSM).

No comments: