Thursday, January 14, 2016

MFUKO WA PPF WASAIDIA KITUO CHA AFYA MISASI.

 Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe, kushoto akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia),msaada wa magodoro 20 na mashuka 20 kwa ajili ya kituo cha Afya Misasi.Kulia ni Happness Manyenye, Ofisa Mwandamizi wa PPFHafla hiyo ilifanyika kituoni hapo jana.
 Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe, kushoto akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia),msaada wa magodoro 20 na mashuka 20 kwa ajili ya kituo cha Afya Misasi.Hafla hiyo ilifanyika kituoni hapo jana.Kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi wa Hlmahsuari ya Misungwi, Nathan Mshana.
PPF Meneja.Meneja wa mfuko PPF,Meshach Bandawe kushotoka akizungunmza na baadhi ya wananchi wa Misasi kabla ya kukabidhi msaada wa magodoro na mashuka kwenye kituo cha Afya Misasi wa pili kutoka kujlia waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye ni Mbunge wa jimbo la Misungwi,kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri wa Misungwi, Nathan Mshana na wa pili ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Khalid Mbitiyaza.
Picha zote na Baltazar Mashaka.

Na Baltazar Mashaka,MWANZA
MFUKO wa Pensheni wa PPF umetatua moja ya changamoto za kituo cha Afya Misasi,Wilayani Misungwi mkoani Mwanza baada ya kutoa msaada wa magodoro 20 na mashuka 20,yenye thamani ya sh.3.5 .

Msaada huo ulikabidhiwa jana kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,hafka iliyofanyika katika kituo hicho na kuhudhuriwa an Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe,alisema mfuko huo umekuwa ukisaidia jitihada za serikali kuboresha afya za jamii kwa kutoa misaada mbalimbali katika sekta ay afya.

Alisema wanafanya hivyo ili kuwasaidia na kuwawezesha wanachama wa mfuko huo wawe na afya bora ili waweze kuchangia kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwakinga na majanga wawapo kwenye ajira.

“Msaada huu wa magodoro 20 na mashuka 20 licha ya kuwa si mkubwa utapunguza changamoto za kituo hiki cha Afya Misasi,na ni sehemu ya kuisadia serikali yetu kuboresha afya za wananchi wake na uwekezaji wa mfuko,”alisema Bandawe

Alimwomba Waziri na Mbunge huyo kuwa, awasaidie kutoa elimu kwa jamii ijunge na mfuko huo ili wanufaike na mafao yanatolewa na PPF kwa kuwakinga na majanga,ili pindi wakistaafua wasipate taabu baada ya kuwa wamekosa nguvu ya kufanya uzalishaji.

“Walimu,Walikuma na Wafugaji wanaweza kujiunga na mfuko kwa ujtaratibu maalum wa kujichangia,hivyo tunakuomba Mbunge utusaidie kutoa elimu kwa wananchi na kuwahamasisha wajiunge na mfuko wetu,”alisema Bandawe.

Naye Kitwanga akipokea msaada huo,aliushukuru mfuko huo akisema umepunguza kero ya magodoro na mashuka lakini pia marafiki zake wa nchini Australia wamesaidia kituo hicho kinachohudumia wilaya tatu za Kwimba, Shinyanga na Misungwi yenyewe, vitanda vya kisasa 16 vyenye thamani ya sh.16 milioni.

Alisema vifaa vizito kulingana na mahitaji ya kituo hicho vinatokana na bajeti ya wilaya kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha tiba bora kwa wananchi zinapatikana kwa karibu.


“Tunahitaji vituo vya Afya kila Kata,hata kituo cha Misasi kinachohudumia baadhi ya vijiji vya wilaya za Shinyanga, Kwimba na Misungwi, kikipanuliwa bado hakitakidhi mahitaji isipokua msongamano utapungua.”alisema

Alisema Serikali itaendelea kuajiri Madaktari na Wauguzi kulingana na bajeti ambapo kwa sasa kituo hicho kina madaktari 14 kutoka wawili wa awali tangu kilipoanzishwa mwaka 1968.

Awali Mganga Mfawidhi wa kituo hicho,Dk.Ernest Celestine alisema kuwa kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa majengo ya wodi wagonjwa wanawake na wanaume wanaofanyiwa upasuaji,magodoro na vitanda,ongezeko la wagonjwa wa huduma za upasuaji,wagonjwa wa nje na wa kulazwa, wagonjwa wa Kifua Kikuu(TB) na Virusi vya Ukimwi (VVU) .


Alisema wanakabiliwa pia na ukosefu wa wodi ya kulala watoto,mashine ya Utra Sound,makazi duni ya watumishi,huduma endelevu za maabara,jengo na jokofu la kuhifadhi maiti,jengo la kuchoma taka hatarishi,jengo la utawala na jiko.

No comments: