Tuesday, January 5, 2016

SUALA LA MAHAKAMA YA MAFISADI NA WAHUJUMU UCHUMI INAFANYIWA KAZI- DKT.MWAKYEMBE

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WAZIRI wa Katiba na Sheria,Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuwa suala la kuanzisha mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi wanafanyia kazi na muda sio mrefu watatoa taarifa juu ya hatua walizofikia. 

Dk.Mwakyembe ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP),amesema kuwa suala mahakama linafanyiwa kazi kwa karibu na ofisi yake kutokana na ahadi ya Rais Dk.John Pombe Magufuli wakati wa kampeni. 

Mwakyembe amesema kuwa watu ambao wanaweza kuleta maendeleo ya nchi ni vyombo vilivyo katika maamuzi ya kisheria hivyo lazima viweze kufanya kazi kwa wananchi kwa kutenda haki. 

Amesema kuwa baadhi ya watendaji wa taaluma ya sheria sio waaminifu kwa kujihusisha na rushwa na kufanya watendaji wote kuharibika kwa sababu ya mtu mmoja. 

Mwakyembe amesema yeye ni mwanasheria na kuongeza kuwa kuna’ majipu’katika tasnia ya taaluma ya sheria na kuwataka majipu hayo yatumbuliwe kabla ya Rais Dk.John Pombe Magufuli hajayatumbua bila sindano ya kupunguza maumivu (Ganzi). 

Mwakyembe amesema kuwa wanajua changamoto ya mawakili wa serikali wanazokumbana nazo ikiwemo miundombinu pamoja na mfumo wa maisha wanayoishi hivyo serikali itafanya uwezeshaji kadri ya uwezo wao. 

Mkurugenzi wa Mashitaka nchini,Buswello Mganga amesema katika mafanikio walioyapata ni pamoja kushinda kesi nane za dawa za kulevya kwa watuhumiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 30.

Mkurugenzi wa mashtaka nchini, Biswelo Mganga akizungumza na kueleza mbambo mbalimbali mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe na kazi walizozifanya ikiwa ni pamoja na kuwashataki wenye hatia za uuzaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Mwendesha mastaka nchini (DPP) na baadhi ya  Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Sheria ikiwemo majumuisho ya ziara ya Sheria na Katiba aliyoifanya hivi karibuni  Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Sheria na Katiba ,Amon Mpanju akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya Waziri wa Katiba na sheria kufanya ziara na kujifunza mambo mbalimbali katika ofisi ya mwendesha mashtaka (DPP).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na wadau wa sheria pamoja na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. kutoka Kulia ni Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Suzan Mlai, Mkurugenzi wa mashtaka nchini, Biswelo Mganga na kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Sheria na Katiba, Amon Mpanju na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome.


Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa toka Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (hawapo pichani) leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments: