Monday, January 25, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AWATUNUKU VYETI WAHITIMU WA CHUO CHA BAHARI

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akizungumza na wahitimu (hawapo pichani) katika mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akimtunuku cheti mmoja kati ya wanafunzi bora waliofanya vizuri katika masomo yao Chuoni hapo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, (wa nne kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo hicho pamoja na baadhi ya wahitimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akionyeshwa Mitambo mipya katika chumba maalum cha kuongozea Meli kutoka kwa Eng. Deizm Mley.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akisaini kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), wakati wa Mahafali ya Chuo hicho. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Yasini Songoro. 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akipata maelezo kutoka kwa Mhandishi wa Meli Stephen Mziray kuhusu utendaji kazi wa mashine mbalimbali za kuongozea Meli.

Wahitimu wa kozi mbalimbali wa Chuo cha Bahari, Dar es Salaam (DMI), wametakiwa kufuata weredi na kufanya kazi kwa bidii ili kukuza uchumi wa nchi ili kufikia lengo la kustawisha pato la kati ifikapo mwaka 2025.

Pia wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi kitaifa na kimataifa sanjari na kuwa waadilifu ili wasiwe majibu na waendane na kasi ya Rais wa awamu ya tano Dk. John Mafuguli katika utendaji kazi na kuwa na uzalendo kwa taifa kwa kutanguliza maslahi ya nchi mbele.

Wahitimu hao pia wametakiwa kujiendeleza kitaaluma ili kuendana na kasi ya mahitaji ya dunia ya sasa kwa lengo la kupambana na soko la ajira kulingana na vigezo vinavyohitajika kitaifa na kimataifa.

Hayo yalizungumzwa juzi jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano, Injinia Joseph Nyamhanga wakati wa mahafali ya 11 ya chuo hicho.

Eng. Nyamhanga alichukua fursa hiyo akimwalisha Waziri wa wizara hiyo Makame Mbarawa ambaye alikuwa katika majukumu mengine ya kiserikali.

Katika mahafali hayo, Eng. Nyamhanga  hakusita kuutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha wanatunza vema vifaa vya kufundishia ili vidumu kwa kipindi kirefu ili ziendelee kutoa huduma ya mafunzo kwa wanafunzi wengine waliopo na watakaojiunga na chuo hicho kwa fani mbalimbali za ubaharia.

Aliongeza kuwa kwa sasa Wizara hiyo inajipanga kwa ajili ya utanuzi wa majengo ya chuo hicho kwa ajili ya kutoa fursa kupunguza changamoto ya ufinyu wa madarasa kutokana na ongezeko la wanafunzi.

Aliongeza kuwa licha ya kuwa katika mchakato huo, eneo la chuo lililoko Mkuranga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam tayari wakazi husika waliokuwa wakimiliki eneo hilo wameshalipwa kwa asilimia 98 hali inayotoa fursa kwa chuo hiyo kujipanga zaidi kuboresha mahitaji ya chuo hicho.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho, Meja Jenerali mstaafu Ligata Sande alisema kuwa chuo kinajipanga kuweka mifumo makini kwa ajili ya maendeleo yanayohitajika sanjari na kutoa wahitimu wenye sifa stahiki watakaoweza kupambana na soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Pia msoma risala kwa upande wahitimu Amani Mshana,  alisema wanafunzi wa DMI wanakabiliwa na changamoto ya kutoshirikishwa kwa katika vikao vya bodi kutokana na kukosekana kwa mwakilishi hali ambayo inasababisha wanafunzi kushindwa kuwasilisha matatizo yao kwenye bodi ya usimamizi wa chuo na kushindikana kutotekelezwa kwa mahitaji yao.

Aliongeza kuwa chuo hicho kina upungufu wa walimu ambapo kwa sasa mwalimu mmoja anafundisha masomo zaidi ya manne na baadhi yao hawana sifa stahiki hususan katika shahada ya kwanza ya uhandisi wa meli na unahodha.

Kutokana na changamoto hizo injinia Nyamuhanga aliwahakikishia wahitimu hao, changamoto hizo kuzifikisha kwa Waziri kwa ajili ya utatuzi. 

No comments: